• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 5:22 PM
Corona ilivyomsaidia kuvuta wateja wa nyama

Corona ilivyomsaidia kuvuta wateja wa nyama

Na MAGDALENE WANJA

Baada ya kujiuzulu kutoka kwa kazi ya uratibu wa miradi katika kampuni moja nchini, Bw Lawrence Waiyaki aliamua kuanzisha biashara ya duka la nyama na mkahawa mjini Limuru.

Ata ivo, biashara hio aliifanya kwa muda wa miaka mitatu kabla ya kuisitisha kutokana na changamototo nyingi katika kazi hio.

Mapenzi yake ya biashara yanatokana na historia ya familia yake ambayo imefanya biashara hii kwa zaidi ya miongo mitatu.

Waiyaki alipozaliwa, familia yao ilikuwa inafanya kazi ya kuchinja na kuuza nyama katika maduka mbalimbali.

“Nilipozaliwa na nilipokuwa mdogo, babu yangu alikuwa na duka kubwa la nyama katika soko ya Dagoretti ambako babangu pia alifanya kazi. Mnamo mwaka 1994, babangu aliacha kazi hio na kufungua duka lake la kuuza nyama,” alisema Waiyaki.

Waiyaki na nduguze walipenda kuandamana na babake kazini na hapo waliweza kujifunza mengi kuhusiana na biashara hio.

Kufikia mwaka wa 1999, baadhi ya watu walioanzisha biashara hio pamoja na babu yake tayari walikuwa na biashara kubwa katika sehemu mbalimbali.

“Niliwaza sana kwa nini babu yangu hakuweza kuendeleza biashara yake kama wenzake walioanza pamoja naye,”alisema Bw Wayaki.

Waiyaki aliamua kurejelea kazi yake tena ila kwa sasa alikuwa akiuza kwa zabuni kwenye mashule na mashirika makubwa.

Japokuwa biashara ile ilimpa faida kubwa, alishindwa kuimudu kwani baadhi ya wateja wake walichelewa kufanya malipo.

Changamoto nyingine kuu aliyopata katika biashara hii ni kuwa ilihitaji mtaji mkubwa kuendesha na hivyo ilimlazimu kutafuta njia mbadala ya kufanya biashara.

Aliamua kuanzisha kampuni ya usambazaji nyama ambayo aliita Nakshi Meat Company katika soko ya Dagoretti.

“Niliamua kufanya biashara ya kuwapelekea wateja wangu nyama katika nyumba zao. Biashara hii ilikuwa na urahisi kufanya kwani wateja wengi walionekana kufurahia mtindo huu,” alisema Waiyaki.

Wakati wa maradhi ya Covid-19, biashara hio iliweza kufanya vyema zaidi kwani watu wengi walisalia makwao. Aliamua kuifanya biashara hiyo kwa upekee kwani ilimpa faida zaidi.

Aliongeza kuwa cha kushangaza ni kwamba, katika kipindi hicho cha mwaka mmoja uliopita, aliweza kupata idadi kubwa zaidi ya wateja.

Nyama anayouza hupakiwa kwenye karatasi za uzani mbalimbali kulingana na hitaji la wateja wake. “Nyama ninayouza imefanyiwa utafiti na kuhakikisha kwamba ina ubora wa kiafya,” aliongeza Bw Waiyaki.

Alisema kuwa anaridhika zaidi katika kazi yake ya kutayarisha na kuuza nyama kwa wateja wake.

You can share this post!

Mwatate United yaendelea kuimarika

WALLAH BIN WALLAH: Tumia Kiswahili kujinyanyua kimaisha,...