• Nairobi
  • Last Updated April 16th, 2024 7:55 AM
KCSE: Waziri aonya wanafunzi wa vyuo

KCSE: Waziri aonya wanafunzi wa vyuo

Na SHABAN MAKOKHA

WAZIRI wa Elimu Profesa George Magoha, amewaonya wanafunzi wa vyuo vikuu dhidi ya kutumiwa na walimu wa shule za upili kuwafanyia watahiniwa wa KCSE mtihani unaonza leo Alhamisi.

Profesa Magoha alisema kuna mpango wa baadhi ya walimu wa shule kushiriki udanganyifu kwa kuwatumia wanachuo ili wanafunzi wao wapate alama za juu.

Alitaja shule za upili zinazopatika katika kaunti za Homa Bay, Migori na Kisii kama zinazopanga kuwatumia wanafunzi wa vyuo vikuu kuiba KCSE.

Kulingana naye, walimu katika shule hizo wamevuruga picha halali za watahiniwa zilizowasilishwa kwa Knec ili wasionekana vizuri kuzuia utambulishi wao.

“Tunafuatilia mienendo ya baadhi ya wasimamizi wa vituo vya kufanya mitihani ambao wanapanga kushiriki wizi wa mtihani,” akasema Profesa Magoha akiwa katika Kaunti ya Busia kukagua mtihani wa KCPE ulivyokuwa ukiendelea.

 

You can share this post!

Barcelona kusajili wanasoka saba wapya baada ya kocha...

CORONA: Uwezo wa chanjo ya China katika kuisaidia Afrika...