• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 9:12 AM
MUTUA: Suluhu aponye madonda aliyoacha Rais Magufuli

MUTUA: Suluhu aponye madonda aliyoacha Rais Magufuli

Na DOUGLAS MUTUA

NIMEREJEA kumuaga aliyekuwa rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli, aliyezikwa Ijumaa.

Amekwenda kutokana na korona, tusidanganyane!

Nilijizuia kutoa ya moyoni tangu alipofariki kwa sababu nilijua Watanzania wengi walikuwa na majonzi kwa msiba huo wa kitaifa.

Lakini kuna Watanzania wengine wengi ambao hawakumpenda kiongozi huyo dhalimu. Hivyo, ni vyema tuambiane tunayoyajua kumhusu, ambayo bado yanawakera. Natumai Rais mpya, Mama Samia Suluhu Hassan, ataiponya nchi.

Kama walivyo madikteta wote, Magufuli alikuwa kiongozi mwoga hivi kwamba labda aliogopa hata kivuli chake. Daima aliishi na hofu ya kusalitiwa na kupinduliwa.

Akitamani kupendwa na kila mtu kwani alijua hakuwa maarufu; hata uteuzi wake wa kuwania urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ulimjia kama bahati tu.

Inaaminika hofu hiyo ndiyo ilimsababisha kuanza kuvunja haki za binadamu mara tu alipoingia ikulu. Dhamira ilikuwa kuwatia woga Watanzania ili wasithubutu kumpinga.

Mwanzoni mwa muhula wa kwanza, Magufuli aliwanyamazisha wanahabari na wanaharakati kwa kuwafunga jela akiapa kuuangamiza upinzani rasmi.

Si ajabu aliwafungulia mashtaka ya kubambikiza wanasiasa wote wa upinzani, na kuwatia hofu wanahabari wasithubutu kuandika chochote kisichomsifia.

Lakini alikosolewa mno na mwanaharakati wa haki za binadamu aliyekuwa pia diwani machachari wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Bw Godfrey Luena.

Marehemu Luena, msemaji mzuri aliyepagawisha wafuasi wake alipopanda jukwaani, aliuawa kwa kukatwakatwa kwa mapanga!

Inadaiwa Magufuli alichoshwa na kelele za Luena ndipo akaamua kumnyamazisha.

Unyama wa Magufuli unajulikana kote duniani kutokana na jaribio la mauaji dhidi ya mwanasiasa mbishi wa upinzani, Bw Tundu Lissu, ambalo lilitibuka kimuujiza.

Bw Lissu, mkali wa kauli na mwepesi wa kufikiria kama mwanasheria, alimkera Magufuli kupindukia kwa kumwita “dikteta uchwara”.

Inadaiwa hilo ndilo lilifanya akafumwa risasi 16 mwilini – kwa jumla zilikuwa 38 zilizomlenga akiwa ndani ya gari lake – zikamvunjavunja mikono, miguu, mbavu na hata sehemu nyeti!

Dikteta hakukoma hapo; alikataza bunge kumlipia Bw Lissu gharama za hospitali; sikwambii hatimaye alimpokonya ubunge wa Sindida Mashariki akitibiwa Ubelgiji.

Utanisadikishaje Mwenyezi Mungu hana mzaha ikiwa aliyenuiwa kuuawa kinyama ameshuhudia msiba wa aliyemkandamiza?

Wakosoaji wengine wakali wa Magufuli ni mwanaharakati Mange Kimambi na mwanasiasa Godbless Jonathan Lema, aliyepokonywa ubunge wa Arusha Mjini kwa kuibiwa kura mwaka jana. Wote walikimbilia Marekani.

Mwanahabari Azory Gwanda alitoweka baada ya kukamatwa na kikosi cha usalama wa taifa alichotumia Magufuli kama jeshi lake binafsi.

Mwanaharakati Ben Saanane, ambaye pia alikuwa msaidizi wa kinara wa Chadema, Bw Freeman Mbowe. Ni miongoni mwa mamia ya vijana waliotoweka kabisa.

Wengine kama mwanahabari Erick Kabendera na mchungaji Zachary Kakobe walizushiwa eti si Watanzania, kwa kukosoa Magufuli.

Dikteta huyo ana bahati kwani ameagwa vyema na nchi nzima, na familia yake wamekubali amewatoka.

Jamaa za wwaliouawa kwa sababu yake hawakupata fursa kama hiyo. Mungu na aziponye nyoyo zao.

Utawala mpya Tanzania uwajibikie maovu ya Magufuli, uuguze na kuponya madonda aliyoachia watu.

[email protected]

Kwa jumla, risasi 38 zililipiga gari lake, lakini 16 zilizompata zilimvunjavunja mikono, miguu, mbavu na hata sehemu nyeti; ndani ya miaka miwili tu ya urais wa Magufuli.

Lissu bado yuko uhamishoni alikokimbilia akihofia kuuawa, baada ya uchaguzi wa mwaka jana aambapo alikuwa mpinzani mkuu wa marehemu.

Wakosoaji wengine wakali wa Magufuli ni mwanaharakati Mange Kimambi na mwanasiasa Godbless Jonathan Lema, aliyepokonywa ubunge wa Arusha Mjini kwa kuibiwa kura mwaka jana. Wawili hao wanaishi Marekani walikokimbilia usalama.

Mhanga mwingine wa Magufuli ni mwanahabari Azory Gwanda aliyetoweka asionekane tena, baada ya kukamatwa na kikosi cha usalama wa taifa alichotumia Magufuli kama jeshi lake binafsi.

Kosa lake? Kuandika habari fichuzi kuhusu ugaidi nchini Tanzania na mapambano dhidi yake. Mkewe, ambaye alishuhudia akikamatwa, bado anamsubiri arejee nyumbani.

Mwingine aliyetoweka kabisa ni mwanaharakati Ben Saanane, ambaye pia alikuwa msaidizi wa kinara wa Chadema, Bw Freeman Mbowe.

Wawili hao ni miongoni mwa mamia ya vijana waliotoweka kabisa. Wapo pia waliotekwa kisha miili yao ikapatikana ikielea kwenye Mto Rufiji au Bahari ya Hindi.

Vilevile, wapo waliobahatika kuachiwa huru baada ya kutekwa na kuteswa kama vile bilionea Mohammed Dewji, mmoja wa watu matajiri zaidi barani Afrika.

Pia msanii wa kizazi kipya, Roma Mkatoliki, aliwahi kutekwa, akateswa na kutupwa barabarani usiku.

Mwanaharakati Tito Magoti alitekwa mara kadhaa na kutupwa vichakani ajifie huko, lakini pepo wa mauti akiifuta miadi kila wakati.

Wengine kama mwanahabari Erick Kabendera na mchungaji Zachary Kakobe walizushiwa ya uraia, si Watanzania eti, wakasingiziwa makosa kwa kumkosoa Magufuli.

Dikteta huyo ana bahati kwa kuwa ameagwa vyema na nchi nzima na familia yake wote wakakubali amewatoka. Jamaa za alioua hawakupata fursa kama hiyo.

Mungu na aziponye nyoyo zao. Utawala mpya wa Tanzania nao uwajibikie maovu ya dikteta huyo, uuguze na kuponya madonda aliyoachia watu.

[email protected]

You can share this post!

TAHARIRI: Heko kwa Harambee Stars kujikaza kisabuni

KAMAU: Sakata ya KCPE ishara uozo bado upo Wizara ya Elimu