• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 9:40 PM
Raia 100 wa kigeni wakamatwa kwa kuwa nchini bila kibali

Raia 100 wa kigeni wakamatwa kwa kuwa nchini bila kibali

Na MARY WAMBUI

POLISI wamewakamata raia 100 wa kigeni kwa kuwa nchini kinyume cha sheria mwezi huu wa Machi pekee. Watu hao wamekamatwa katika kaunti za mpakani za Garissa, Isiolo, Tana River, Wajir na Mombasa huku wengine wakimatwa katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.

Kulingana na habari zilizoonekana na Taifa Leo, wengi wa raia hao wanatoka Burundi, Somali na Ethiopia na wachache wanatoka Msumbiji na Ufilipino.

Mwanzoni mwa mwaka huu, raia watano wa Burundi waliotambuliwa kama Akumuremyi Dancile, Kanyambo Zaitun, Habonimana Noeza, Barakamfitiye Vumiliya na Ndunimana Angele walikamatwa katika uwanja wa ndege wa JKIA na polisi walisema hawakuweza kueleza kwa nini walikuwa nchini.

Maafisa wa idara tofauti katika uwanja huo wa ndege waliwawasilisha kwa idara ya uhamiaji iwachukulie hatua zaidi.Siku iliyofuata katika eneo la Bamburi, kaunti ya Mombasa, raia wanne wa Ufilipino waliotambuliwa kama Canete Ronaldo Gaylan, palaganas Eduardo Suarez, Panares Renante Guylan na Mervin Magallanes walikamatwa na maafisa wa kulinda wanyama pori wakishiriki uvuvi bila leseni.

Siku hiyo, maafisa wa usalama kaunti ya Kitui walimkamata mwanamke raia wa Somalia kwa jina Kafiyo Ahmed Mocow 25, akiwa na kitambulisho kilichokuwa na jina la mtu mwingine.

Mwanamke huyo alikuwa akielekea Nairobi kutoka Garissa.Mnamo Machi 4, kundi la maafisa wengine wa usalama katika kizuizi cha barabarani Merti kwenye barabara ya Isiolo kwenda Moyale walimkamata mwanamke kwenye umri wa miaka 17 raia wa Ethiopia akielekea Nairobi kutoka Moyale.

You can share this post!

Maamuzi tofauti ya korti yaibua utata kesi ya polisi

DHULUMA ZA KIMAPENZI: Serikali yaitia adabu Homeboyz Radio