• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 3:04 PM
Watu 45 walifariki katika makanyagano wakitazama mwili wa Magufuli, polisi wa TZ hatimaye wakiri

Watu 45 walifariki katika makanyagano wakitazama mwili wa Magufuli, polisi wa TZ hatimaye wakiri

Na MWANGI MUIRURI

MAAFISA wa usalama katika Jamuhuri ya Tanzania sasa wamekiri kuwa takriban watu 45 waliaga dunia katika hafla ya kuutazama mwili wa Rais Joseph John Pombe Magufuli mnamo Machi 21.

Watano kati ya mauti hayo yalihusisha wa kutoka familia moja na ambao tayari walizikwa wiki jana.

Hali hiyo imesemwa na kitengo hicho cha usalama kwamba ilizuka wakati maelfu ya waombolezaji walijitokeza katika uwanja wa Uhuru ulioko Mjini Dar es Salaam na ambapo kulizuka msukumano ulioishia mkannyagano, kwa kimombo ikiwa ni stampede.

Wengine 37 wameripotiwa kuwa walipata majeraha ya viwango mbalimbali, hali hiyo ikionyesha mapenzi wengi walikuwa nayo kwa mwendazake ambaye alihudumu kama rais wa traifa hilo kwa miaka sita akiwa rais wa tano.

Ni uongozi ambao wengi wameupa wasifu wa kujituma kukabiliana na changamoto za umasikini, ufisadi na utepetevu huku aking’ang’ania kuwakinga Watanzania kutokana na ushindani usio na usawa katika safu za biashara ndani ya JUmuia ya Afrika Mashariki.

Pia, aloisifiwa kama rais aliyekuwa na imani thabiti ndani ya Ukristo wa Kikatoliki na ambapo aliwatuma watu wake kumtegemea Mola katika hali zao zote za changamoto—virusi vya Corona vikiwa ni miongoni mwa majanga ambayo aliwaelekeza raia wa Tanzania wavikabili kupitia maombi na ganga za kitamaduni.

Kwa sasa, majukumu ya urais yamekabidhiwa aliyehudumu kama Naibu wa Rais wa mwendazake, Bi Samia Suluhu.

Kwa mujibu wa Kamanda wa kikosi cha walinda usalama cha Mji wa Dar Bw Lazaro Mambosasa, akiongea na waandishi wa habari wa jarida la Mwananchi alisema kuwa hali hiyo ya mauti ilikuwa ya kuhuzunisha.

“Hao watu walioaga dunia hawakuwa majambazi. Walifika tu kwa uwanja kuonyesha mapenzi yao na huzuni kwa kiongozi wao aliyevunwa na mkuki wa mauti,” akasema.

Magufuli aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 61.

Aliongeza kuwa uwanja huo Mwili wa Magufuli ulikuwa umewekwa kwa harakati hizo za utazamaji ulikuwa na nafasi finyu kwa maelfu ya waliokuwa na hamu ya kuupa heshima za mwisho kabloa ya kuzikwa katika eneo la Chato.

Ndipo, akaongeza, wengine waliishiwa na subira ya kufanikiwa kuufikia mwili wautazame na wakaamua kutumia viingilio mbadala ambavyo havikuwa na utaratibu hali iliyoishia kuzuka kwa patamshike ya mauti kwa raia hao.

You can share this post!

China yaanza kutoa chanjo ya Covid-19 kwa wageni wa mataifa...

Corona ilivyoyasukuma makanisa kuchangamkia teknolojia