• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:33 AM
Pasaka chungu kwa wakazi wa kaunti tano

Pasaka chungu kwa wakazi wa kaunti tano

Na MARY WAMBUI

WAKAZI wa kaunti tano za Nairobi, Kiambu, Machakos, Kajiado na Nakuru watasherehekea sikukuu ya Pasaka bila mbwembwe.

Hii ni kutokana na kuwa wakazi hao wapatao milioni 12, hawawezi kusafiri nje ya eneo lililotengwa ili kuzuru mashambani ama kmaeneo ya kitalii kama ambavyo imekuwa miaka ya awali.

Hii ni baada ya Rais Uhuru Kenyatta wiki iliyopita kuweka kaunti hizo chini ya marufuku kwa kile alichosema ni katika juhudi za kuzuia kusambaa kwa ugonjwa wa Covid-19.

Hapo jana, Inpekta Jenerali wa Polisi, Hilary Mutyambai alisema vizuizi 33 vilikuwa vimewekwa katika kaunti hizo tano ili kuwazuia raia kuingia au kutoka katika kaunti hizo.

“Tunajua watu wengi watakuwa wakisafiri nyumbani ili kuungana na familia zao kwa sherehe za Pasaka. Hata hivyo, ningependa kuwarai wanaoishi katika kaunti hizo zilizofungwa wasiondoke isipokuwa wale wanaotoa huduma spesheli,” akasema Bw Mutyambai.

Kulingana na marufuku hiyo, wakazi hao pia hawawezi kuzuru maeneo ya burudani baada ya mikahawa na baa kufungwa. Pia hawawezi kufanya karamu za kijamii kwani mikusanyiko pia imeharamishwaHapo jana, Rais Kenyatta alitetea hatua ya kufunga kaunti hizo tano akisema ni kwa manufaa ya kulinda maisha ya wananchi.

Alisema kuwa marufuku hiyo sio adhabu mbali alitenda kwa ushauri wa wataalamu wa afya.Wakati huo huo, serikali imejikanganya tena kuhusu kafyu iliyowekwa kama mojawapo ya masharti ya kuzuia kuenea kwa virusi vya corona.

Mnamo Ijumaa wiki iliyopita, Rais Kenyatta alibadilisha saa ya kafyu kutoka saa saa nne usiku hadi saa mbili za jioni katika kaunti tano ambazo zilifungwa.

Kauli ya Rais jana iliungwa mkono na Bw Mutyambai ,ambaye alisema kuwa kafyu katika kaunti hizo tano itabakia kuanzia saa mbili usiku na kwingine saa nne.Awali Wizara ya Usalama ilisema kafyu itaanza saa mbili kote nchini.

You can share this post!

UHURU AMTULIZA RAILA

Abdul Haji afuata nyayo za waliorithi jamaa zao kisiasa