• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
Chanjo ya AstraZeneca yaua watu saba

Chanjo ya AstraZeneca yaua watu saba

Na AFP

WATU saba kati ya 30 walioathirika na kuganda kwa damu baada ya kupewa chanjo ya AstraZeneca walifariki, halmashauri ya matibabu nchini Uingereza imefichua.

Ufichuzi huo unajiri wakati ambapo mataifa kadha ya Uingereza yamesitisha shughuli za utoaji wa chanjo aina ya AstraZeneca kuhusiana na madhara ya kuganda kwa damu miongoni mwa baadhi ya watu waliochanjwa.

“Kati ya visa 30 vilivyoripotiwa vya watu kuganda damu kufikia Machi 24, inasikitisha kuwa saba wamefariki,” ikasema halmashauri ya Kusimamia Dawa na Bidhaa za Kimatibabu nchini Uingereza.

Mnamo Ijumaa, taifa la Uholanzi lilisitisha utoaji chanjo ya AstraZeneca kwa watu wenye umri wa chini ya miaka 60 baada ya visa vya wanawake watano kuathiriwa na mgando wa damu kuripotiwa. Baadaye mmoja wa wanawake hao alifariki.

Ujerumani ulichukua hatua sawa na hiyo mapema wiki hii.Shirika la Dawa Barani Uropa (EMA) ambalo sawa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), lilishikilia kuwa chanjo ya AstraZeneca ni salama, linatarajiwa kutoa taarifa nyingine kuhusu suala hilo mnamo Aprili 7.

 

You can share this post!

Wakristo wakosa mbwembwe za Pasaka corona ikiwafungia

Mbunge ataka sheria ya kudhibiti nchi kufungwa