• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 2:08 PM
Wakiukaji 1,600 wa masharti ya corona wanaswa Murang’a wakisherehekea Pasaka ndani ya mtindi

Wakiukaji 1,600 wa masharti ya corona wanaswa Murang’a wakisherehekea Pasaka ndani ya mtindi

Na MWANGI MUIRURI

WASHUKIWA 1,600 walinaswa katika Kaunti ya Murang’a wakikiuka masharti ya Covid-19 ndani ya uraibu wa pombe eti wanasherehekea Pasaka.

Walitiwa mbaroni katika kaunti zote ndogo nane za kaunti hiyo katika vituo vya polisi 240.  Walikuwa wakisherehekea sikukuu hiyo ambayo kwa Wakristo huwa ni ya kukumbuka kusulubiwa kwa Yesu Kristo kutoa fursa kwa waumini kuokolewa kutoka kwa dhabi. Lakini kwao sherehe ilikuwa ni ulevi.

Katika takwimu 1,200 walinaswa katika Kaunti ndogo zote nane za Kaunti hiyo wakiwa wamefungiwa ndani ya baa baada ya saa tatu za usiku.

Masharti ya huduma za baa katika Kaunti 42 ni kwamba baa zote ziwe zikifungwa saa tatu, lakini katika kaunti za Nakuru, Nairobi, Machakos, Kiambu na Kajuado huduma za baa zikiwa ni marufuku.

Katika msako wa Murang’a, watu 300 zaidi walinaswa wakisuasua mitaani wakiwa walevi pamoja na wengine ndani ya idadi hiyo wakiendesha magari yao wakiwa walevi baada ya saa nne ambayo ni wakati wa kuanza kwa kafyu.

Hao wengine 100 walinaswa katika misako dhidi ya magweni ya uuzaji Pombe haramu katika Kijiji cha Maica Ma Thi Kilichoko katika Kaunti ndogo ya Murang’a Kusini.

Lita 160 za pombe hiyo zilinaswa.

Kamishna wa Kaunti Bw Mohammed Barre alisema kuwa msako huo utazidishwa kwa mujibu wa masharti ya Covid-19 sambamba na mikakati ya kawaida ya kutekeleza sheria.

Alisema kuwa washukiwa wote waliokamatwa walipewa dhamana kwa mujibu wa masharti ya Covid-19 ambayo yanahitaji vituo vya polisi vijiepushe na misongamano itakayoishia hatari ya maambukizi kutanda hadi mahakamani na magereza.

Bw Barre alisema kuwa wote watakaonaswa watapewa Kazi za kudumisha usafi mtaani.

Aidha, Bw Barre alionya maafisa wa Polisi wanaothibiti kizuizi cha kuzima utangamano wa Kaunti za Kiambu na Murang’a karibu na Mji wa Thika wajiepushe na ufisadi unaoripotiwa kukubalia watu kuingia na kutoka katika kizuizi hicho.

Bw Barre alisema kuwa ako na ufahamu wa wahudumu wa bodaboda ambao wanahepeshea abiria katika shamba la mananasi la Del Monte na kuwaingiza au kuwatoa Mjini Thika hivyo basi kumhujumu maana na lengo katika kizuizi hicho.

You can share this post!

Wachuuzi wa vyakula Ruiru walalamika

Askofu Muheria awataka machifu na maafisa wa polisi...