• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 10:40 AM
Zaidi ya wafungwa 1,800 watoroka baada ya shambulio la gereza Nigeria

Zaidi ya wafungwa 1,800 watoroka baada ya shambulio la gereza Nigeria

Na MASHIRIKA

OWERRI, Nigeria

ZAIDI wa wafungwa 1,800 walitoroka kutoka kwa gereza moja nchini kufuatia shambulio la watu wenye silaha hata zikiwemo gudunedi, bunduki na vilipuzi.

Washambuliaji hao walitumia vilipuzi kubomoa ua la ukuta wa gereza hilo lililoko katika mji wa Owerri kabla ya kuingia ndani. Mji wa Owerri uko umbali wa karibu kilomita 400 kusini mashariki mwa jiji kuu nchini Nigeria, Lagos.

Idara ya Magereza Nchini Nigeria ilithibitishia wanahabari kwamba jumla ya wafungwa 1,844 walitoroka baada ya shambulio hilo lililotokea Jumatatu.

Polisi nchini Nigeria walidai kuwa shambulio hilo lilitekelezwa na wafuasi wa kundi la wapiganaji kwa jina Indigenous People of Biafra (IPB).

Hata hivyo, shirika la habari la AFP limeripoti kwamba kundi hilo limekana kuhusika katika shambulio hilo.

Vituo kadha vya polisi vimeshambaliwa kusini na watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa makundi ya kigaida nchini Nigeria tangu Januari mwaka. Wavamizi hao pia wamekuwa wakiiba idadi kubwa ya bunduki katika mashambulio hayo.

Hata hivyo, hakuna makundi yamedai kuhusika katika mashambulio hayo, kulingana na ripoti za vyombo vya habari.

TAFSIRI: CHARLES WASONGA

You can share this post!

Mkopo wa IMF wazua hasira kwa Wakenya

Serikali yanyonga wanyonge