• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
Mwanamume aliyeonekana akiteswa kwa kuchomwa na chandarua kinachoteketea kupitia video ajitokeza

Mwanamume aliyeonekana akiteswa kwa kuchomwa na chandarua kinachoteketea kupitia video ajitokeza

Na SAMMY WAWERU

MWANAMUME aliyenakiliwa kupitia kanda ya video akiteswa kwa kuchomwa na chandarua cha mbu hatimaye amejitokeza.

Kufuatia video inayosambaa mitandaoni, mshukiwa wa kitendo hicho cha unyama ambaye ametambuliwa kama Swabir Abdul Razaq Mohamed alikamatwa Jumatatu na maafisa wa Idara ya Uchunguzi wa Jinai (DCI) Mombasa.

Hata ingawa video hiyo haijulikani ilinakiliwa lini ili kubaini siku ya tukio, mwathiriwa amesema alitendewa ukatili na mfanyakazi wa kampuni moja Mombasa wakati akienda kutafuta kazi.

“Alitendea dhuluma kwa madai nilikuwa mwizi ilhali nilikuwa nimeenda kuomba ajira,”akaelezea.

Alisema aliuguza majeraha, na tangu tukio hilo lifanyike amekuwa akitegemea wasamaria wema kukithi riziki na mahitaji muhimu ya kimsingi.

“Niliumia kichwani, ambapo nilipata majeraha yaliyonilazimu kushonwa. Nimekuwa ombaomba tangu nidhulumiwe,”akasimulia.

Kwenye video, anaonekana kufungwa kwa kamba kwenye kikingi, mshukiwa akimchoma kwa chandarua cha kuzuia mbu kinachoteketea.

“Nilipotaka kuenda kumripoti kwa polisi nilionywa na marafiki zangu kuwa ni mtu tajiri, sitapata haki kwa sababu atawahonga maafisa watupilie mbali malalamishi yangu,” akasema.

Mwathiriwa huyo hata hivyo ameelekea katika kituo cha polisi kuandikisha taarifa, baada ya DCI kuhimiza ajitokeze haki ipatikane.

Tukio hilo la kikatili limezua hasira na mjadala mkali mitandaoni, wachangiaji wakitaka mshukiwa achukuliwe hatua za kisheria mara moja.

  • Tags

You can share this post!

Wakenya waomboleza rais wa mchezo wa kuogelea Kenya (KSF)...

Wanaoenda kuhiji Mecca kuhitaji cheti cha chanjo