• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 8:55 AM
Shirika laonya kuhusu nyama

Shirika laonya kuhusu nyama

Na MWANDISHI WETU

NYINGI ya nyama ya nguruwe na kuku inayouzwa katika maduka makubwa nchini sio salama kwa afya ya binadamu.

Kulingana na Shirika la Kulinda Wanyama Duniani, sampuli za nyama kutoka maduka katika kaunti za Nairobi, Kisumu, Nakuru, Laikipia, Uasin Gishu na Nyeri zilionyesha kuwa asilimia 98 ya nyama ya nguruwe ilikuwa na viini vya bakteria ilihali asilimia 97 ya kuku ilikuwa na viini hivyo vinavyosababisha maradhi.

Uchunguzi huo pia ulionyesha kuwa asilimia 38 ya bakteria hao ni sugu kwa dawa za kuwaua.

“Hii inatokana na matumizi ya dawa za kuua bakteria kwa mifugo. Uchunguzi umeonyesha kuwa asilimia 70 ya dawa za bakteria zinazoingizwa nchini zinapewa nguruwe, kuku na ng’ombe,” ikasema taarifa kuhusu hali ya usalama wa nyama nchini.

Wataalamu sasa wanapendekeza kuchukuliwa kwa hatua za kupunguza matumizi ya dawa kwa mifugo kwa kuhakikisha usafi wa mazingira ya mifugo, kuwapa chakula kifaacho pamoja na matumizi ya chanjo kuzuia magonjwa.

You can share this post!

18 wafariki kwenye ajali mbili tofauti Kisumu, Kilifi

Ubakaji wakithiri kwa wanawake wakihepa kafyu