• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 5:22 PM
Rais Suluhu Hassan abuni kamati ya Covid-19

Rais Suluhu Hassan abuni kamati ya Covid-19

Na THE CITIZEN

DAR ES SALAAM, Tanzania

RAIS wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Jumapili alibuni kamati ya wataalamu ili imshauri kuhusu hali ya Covid-19 nchini humo na hatua ambazo anapaswa kuchukua kupambana na janga hilo.

Kiongozi huyo alitoa wito kwa viongozi wa kidini kutoa hamasisho kuhusu ugonjwa huo ili waumini wao wachukue tahadhari za kujikinga kama vile kunawa mikono kwa sabuni kwa maji yanayotiririka, kutumia sanitaiza, kuvalia barakoa na kutokaribiana sana.

Alisema hayo jijini Dodoma wakati wa kongamano la kitaifa lililoandaliwa na viongozi wa kidini kumkumbuka rais wa zamani Hayati John Pombe Magufuli na kuombea viongozi wapya akiwemo yeye na mwenzake wa Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi.

Rais Hassan alisema kuwa ugonjwa huo umekuwa ukisaambaa na aina mpya ya virusi vya corona kuripotiwa sehemu mbalimbali duniani.

“Nilivyoahidi wakati wa kuapishwa kwa makatibu wa wizara na manaibu wao, tayari nimebuni kamati ya wataalamu kuhusu Covid-19. Natarajia kukutana na wanachama wake na wawakilishi kutoka Wizara ya Afya na Wizara ya Fedha ili kutoa mwelekeo,” akasema.

Rais huyo alisema kuwa ingawa athari za ugonjwa huo sio kubwa nchini Tanzania, sio vizuri kupuuzilia uwepo wa ugonjwa huo nchini humo.

“Ningependa kuahidi kuwa nitakuwa nikipokea habari za kila siku kuhusu ugonjwa huo kutoka kwa kamati hiyo ili kuokoa taifa dhidi ya raia kufariki na kuwalinda wale wanaokabiliwa na hatari ya kuambukizwa Covid-19,” Bi Hassan akaeleza.

Tafsiri: CHARLES WASONGA

You can share this post!

Waume wazomea pasta wa wake wao

Raila chaguo la Uhuru 2022 – Murathe