• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 7:55 AM
Hatuogopi yeyote, wanavoliboli wa KPA wajipiga kifua baada ya kuingia robo-fainali ya Afrika

Hatuogopi yeyote, wanavoliboli wa KPA wajipiga kifua baada ya kuingia robo-fainali ya Afrika

Na GEOFFREY ANENE

WASHIRIKI wapya KPA wamesema hawaogopi yeyote kwenye mashindano ya Afrika ya klabu za voliboli za wanaume yanayoendelea jijini Tunis, Tunisia.

Katika mahojiano na Taifa Leo baada ya KPA kufuzu kushiriki robo-fainali na kukutanishwa na Zamalek, kocha Mkuu Sammy Mulinge amesema Jumatano watajikakamua vilivyo kushinda Wamisri hao.

“Kwanza kabisa, napongeza juhudi ambazo wachezaji wangu wameonyesha. Tuliweka lengo, tukatafuta mbinu ya kulitimiza na hatimaye tuko katika robo-fainali. Inafurahisha kuwa wachezaji wamefika hatua hii katika mara ya kwanza ya klabu hii kushiriki mashindano haya. Nimefurahishwa na matokeo haya. Tulikuwa na mpango wa mechi hii, kimbinu na kiufundi. Tulifanya kazi kubwa kujiandaa kiakili kwa mashindano ya kiwango cha juu na timu ambazo mashindano haya ni kawaida kwao. Tumeona matunda na tunahisi kuridhika,” alisema Mulinge baada ya KPA kuzaba APR (Rwanda) 3-2 na Rukinzo (Burundi) 3-0 na kupoteza 3-0 dhidi ya wenyeji na mabingwa wa mwaka 1994, 1998, 2000 na 2014, Esperance.

“Mechi yetu ijayo ni dhidi ya Zamalek. Tunawaheshimu kwa sababu wanajivunia mataji matano (1984, 1987, 2008, 2009 na 2012). Hata hivyo, hatuogopi mtu yeyote. Tutajipigana kufa-kupona kutafuta matokeo mazuri. Tunataka matokeo mazuri katika michuano iliyobaki,” aliongeza kocha huyo anayeshikilia pia wadhifa wa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Kenya ya voliboli ya ufukweni.

Mulinge alishukuru maafisa wa ngazi ya juu wa kampuni ya KPA wakiongozwa na Meneja Mkuu wa Ajira na Usimamizi Daniel Ogutu akisema usaidizi wao wa hali na mali kwa timu hiyo wakati wa michuano hiyo umechangia katika ufanisi wao. “Hao ndio nguzo wa timu hii. Pia, Short or long biceps: what a difference in bodybuilding testo cypmax buy bodybuilding anabolic steroid testosterone undecanoate, testosterone cure buy – freeroll-passwords. benchi yote ya kiufundi ya KPA imefanya kazi nzuri katika safari yetu ya kufika robo-fainali. Tunasubiri kwa hamu kubwa mchuano huo tukiwa na matumaini ya kufanya vyema. Nani amesema haiwezekani?” aliuliza.

Katika mashindano hayo, Kenya pia inawakilishwa na GSU ya kocha Gideon Tarus ambayo italimana na Esperance katika robo-fainali nyingine.

You can share this post!

Vissel Kobe anayochezea Masika yalimwa Kombe la Levain,...

Kenya, DRC zatia saini mikataba ya kuimarisha ushirikiano