• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
Serikali ya TZ sasa yaweka mitambo ya oksijeni hospitalini

Serikali ya TZ sasa yaweka mitambo ya oksijeni hospitalini

Na Mashirika

TANZANIA imeweka mitambo ya kuzalisha oksijeni katika hospitali zake za kitaifa kuwasaidia katika matibabu ya wagonjwa wa Covid-19, Wizara ya Afya ilisema Ijumaa.

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, wizara hiyo ilisema kuwa mitambo ambayo itawekwa katika kila hospitali saba za rufaa, itakuwa na uwezo wa kuzalisha mitungi 200 ya oksijeni kwa siku.

Tangazo la kuwekwa kwa mitambo hiyo katika mradi unaodhaminiwa na Benki ya Dunia ni hatua nyingine ya Tanzania kubadili sera yake kuhusu Covid-19 tangu kufariki kwa Rais John Pombe Magufuli mnamo Machi mwaka huu.

Mapema mwezi Aprili Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alibuni kamati ya wataalamu ambao aliwatwika wajibu wa kushauri mkondo ambao Tanzania inafaa kufuata katika vita dhidi ya janga hilo, sambamba na inavyofanyika ulimwenguni.

You can share this post!

Washukiwa 11 wa kundi la MRC waliokamatwa wachunguzwa

Wagonjwa 18 wa corona wafa moto ulipozuka kwenye wodi