• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 5:46 PM
Waomba serikali isiruhusu uuzaji wa nyama ya punda

Waomba serikali isiruhusu uuzaji wa nyama ya punda

NA VITALIS KIMUTAI Na JACOB WALTER

Wamiliki wa punda eneo la Kusini mwa Bonde la Ufa wameomba serikali isiondoe marufuku ya kuchinja na kuuza nyama ya mnyama huyo.

Mahakama iliondoa marufuku ya biashara ya nyama ya punda na wamiliki hao wanasema kuhalalishwa kwake kutafanya wizi wa wanyama hao eneo hilo ambao ulikuwa umewasababishia hasara kubwa kurejea.

“Tunaomba mashirika ya kutetea maslahi ya wanyama na wasamaria wema kutuokoa kwa kurudi kortini kupinga uamuzi huo,” alisema mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa Punda.

Jaji Richard Mwongo aliondoa marufuku hiyo baada ya serikali kukataa kujibu kesi iliyowasilishwa na kampuni ya Star Brilliant kupinga ilani yaWaziri wa Kilimo, Peter Munya aliyoharamisha biashara ya nyama ya punda Kenya.

Star Brilliant ilisema katika kesi yake kwamba, ilani ya Bw Munya ilikiuka haki za kampuni hiyo na ilifaa kuondolewa. Wamiliki wa punda walisema watu wengi walipoteza wanyama wao kwa wezi wa mifugo.

You can share this post!

Spika atangaza nia ya kumrithi Gavana Mutua

Wakazi walala msituni wakihofu kukamatwa