• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 6:50 PM
Wakazi walala msituni wakihofu kukamatwa

Wakazi walala msituni wakihofu kukamatwa

Na Alex Njeru

BAADHI ya wanakijiji wa Kithioroka, Tharaka-Kusini wanaendelea kulala misituni ili kuwaepuka polisi wanaolenga kuwakamata wahalifu walioharibu mali ya thamani ya Sh2 milioni ya raia kutokana na mzozo wa ardhi.

Tayari wanakijiji 27 wanaoshukiwa kuteketeza nyumba na kuua mifugo ya Nthante Ndereba mnamo Machi 25, 2021, wakimshutumu kwa kunyakua ardhi ya shule ya msingi ya Kithioroka, wamekamatwa.Washukiwa hao walifikishwa katika mahakama ya Marimanti na kuachiliwa kwa dhamana ya Sh1 milioni kila moja.

Kamanda wa polisi wa Tharaka Kusini Kiprop Rutto hata hivyo amewaondolea hofu akisema maafisa wa usalama wanalenga tu wahalifu wala si kila raia.

Hata hivyo, Bw Ndereba amemshutumu mbunge wa Tharaka Gitonga Murugara kwa kuwachochea wanakijiji kuharibu mali yake kwa kisingizio kuwa amenyakua ardhi ya shule. Anadai mbunge huyo aliwachochea wakazi wakati wa mkutano na hata kuahidi kuchangisha pesa za kujenga ua wa shule.

 

  • Tags

You can share this post!

Waomba serikali isiruhusu uuzaji wa nyama ya punda

Joho, Ruto waua ndoto ya chama cha Wapwani