• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 AM
Wanafunzi wawili wa MKU wapata ufadhili kwa ubunifu wao kibiashara

Wanafunzi wawili wa MKU wapata ufadhili kwa ubunifu wao kibiashara

Na LAWRENCE ONGARO

WANAFUNZI wawili wa Chuo Kikuu cha Mount Kenya (MKU) ni miongoni mwa watu 750 wabunifu wa njia mbalimbali za biashara waliopokea ufadhili wa kujiendeleza.

Wanafunzi hao wamenufaika na ufadhili kupitia mpango wa Mbele Na Biz ulioendeshwa na serikali kupitia wizara husika.

Bw Christopher Arunga wa somo la biashara MKU, alipokea ufadhili wa Sh3.6 milioni kwa ubunifu wake wa kuunda mtambo wa kutengeneza chakula cha mifugo katika Kaunti ya Kakamega.

Naye Kangethe Sylvia Wanjiku ambaye ni mwanafunzi wa maswala ya ununuzi na uuzaji wa bidhaa, alipokea ufadhili wa Sh900,000 kwa ubunifu wake wa kustawisha biashara ya chokoleti katika Kaunti ya Murang’a.

Wawili hao walipata ujumbe kutoka kwa afisi kuu ya MKU kuwajulisha kuwa wameteuliwa kuwa miongoni mwa watu wabunifu katika kitengo cha biashara.

Wawili hao walipohojiwa walikiri ya kwamba ubunifu wao ulikuwa muhimu kutokana na maono yao ya siku zijazo.

Katika ushindani wa kibiashara, watu 11,000 walishiriki huku 750 wakiteuliwa miongoni waliofanikiwa.

MKU iko katika mstari wa mbele kuwakuza wanafunzi wanaojihusisha na masomo ya biashara kupitia ubunifu chini ya mwavuli wa Graduate Enterprise Academy (GEA).

Lengo la mpango huo ni kuona ya kwamba mwanafunzi yeyote anayepitia chini yao ni sharti awe na ari ya kujitegemea mwenyewe baada ya kukamilisha masomo yake.

Hatua hiyo imeiweka MKU kwenye ramani ya masomo kwa sababu wanafunzi wengi kupitia vitengo tofauti vya elimu wanaonyesha ubunifu wa hali ya juu.

You can share this post!

Kagwe adai shirika lilitaka kukwepa ushuru wa dawa za HIV

Kilifi Ladies FC yaomba kushiriki ligi ya Pwani