• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 9:12 AM
CHARLES WASONGA: Elimu eneo la Kaskazini mwa Kenya iimarishwe

CHARLES WASONGA: Elimu eneo la Kaskazini mwa Kenya iimarishwe

Na CHARLES WASONGA

SERIKALI kuu inapaswa kukabiliana na changamoto zinazoathiri viwango vya elimu katika maeneo ya kaskazini mwa Kenya ambayo yamekuwa yakiandikisha matokeo duni kila mwaka.

Kuimarika kwa elimu ndiko kutawazesha maeneo hayo kupiga hatua kimaendeleo ikizingatiwa kuwa yamesailia nyuma tangu taifa hili lilipopata uhuru wa kujitawala mnamo 1963.

Kwa mfano, inasikitisha kuwa katika matokeo ya mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne (KCSE 20202) yaliyotangazwa mnamo Jumatatu wiki hii, hamna mwanafunzi aliyepata gredi ya A katika baadhi ya kaunti za kaskazini mwa nchi na pwani.

Kaunti hizo ni; Mandera, Wajir, Marsabit, Garissa, Isiolo, Tana River, Kilifi na Lamu ambazo zimezongwa na matatizo ya kudorora kwa usalama, uhaba wa walimu, ukame, njaa na athari za tamaduni zilizopitwa na wakati kama vile ukeketaji wa wasichana.

Kwa hivyo, ingawa elimu inapaswa kuleta usawa katika jamii yoyote ile, changamoto hizo zimedunisha masomo katika maeneo hayo kiasi cha kuchangia wakazi kuingiwa na hisia kwamba kaunti zao sio sehemu ya Kenya.

Kwa mfano, katika kaunti ya Garissa mwanafunzi aliyepata gredi ya juu zaidi ya A- alikuwa Abdikadir Salat Mohamed kutoka Shule ya Upili ya Gedi huku aliyefanya vizuri zaidi katika kaunti ya Mandera alipata gredi ya B+.

Huyu ni Mahat Abdi kutoka Shule ya Upili ya Mandera.Katika kaunti za Tana River, Kilifi na Lamu ripoti za vyombo vya habari zinasema viwango vya somo vimeshuka kwa sababu shule nyingi za upili zimeathirika na kodorora kwa usalama, uhaba wa walimu na ukosefu wa miundo msingi.

Kwa mfano, ingawa Shule ya Upili ya Wavulana ya Hola na Shule ya Upili ya Wasichana ya Ngao katika kaunti ya Tana River zilipandishwa hadhi ya kuwa shule za kitaifa miwili iliyopita, ziliandikisha alama za wastani za 3.0 na 2.7 mtawalia katika mtihani wa KCSE wa 2020.

Nimetoa taaswira hii kushadidia himizo langu kwa serikali kwamba inapaswa kujitwika wajibu wa kuingilia kati ili kuinua viwango vya masomo katika maeneo hayo.

Walimu wahakikishiwe usalama ili wawe na moyo wa kuendelea kuhudumu katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Kenya. Mnamo 2019, zaidi ya walimu 200 kutoka maeneo mengine ya nchi waliokuwa wakifunza katika eneo pana la kaskazini mashariki mwa Kenya walihama baadhi ya wenzao watatu kuuawa katika mashambulio ya kigaidi.

Vile vile, serikali ichimbe visima na mabwawa katika maeneo hayo kame ili jamii za wafugaji ziweze kupata lishe na maji kwa mifugo wao. Hii itawafanya watu hao kukoma kuhamahama kila mara kusaka lishe, hali inayovuruga maisha ya jamii za maeneo hayo, haswa masomo ya watoto wao.

Ukweli ni kwamba kuna wanafunzi wengi kutoka maeneo hayo wanaweza kupata gredi za A katika mtihani wa KCSE na ule wa kitaifa wa darasa la nane (KCPE) lakini changamoto hizi ndizo zimewadumaza kielimu.

Kwa mfano, nina uhakikka kwamba mtihaniwa kama vile Mahat Abdi wa Shule ya Upili ya Mandera, aliyepata gredi ya B+ katika mazingira magumu eneo hilo, anaweza kupata gredi ya A katika mazingira faafu katika maeneo mengine ya nchi.

You can share this post!

BENSON MATHEKA: Serikali iweke sera kulinda watoto wenye...

Ajabu ya shule moja kuandikisha ā€˜Eā€™ kwenye masomo yote...