• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 8:12 PM
WANYAMA: BBI: Uamuzi wa korti waweza kukosolewa

WANYAMA: BBI: Uamuzi wa korti waweza kukosolewa

Na PETER WANYAMA

MNAMO Mei 14, 2021, majaji watano wa Mahakama Kuu walitoa uamuzi wa pamoja wa kuzima Mswada wa Marekebisho ya Katiba wa 2020 uliotokana na Jopokazi la Mpango wa Maridhiano (BBI) lililobuniwa na Rais Uhuru Kenyatta.

Hukumu hiyo imesifiwa kama ‘uamuzi wa karne’ kwa sababu ya athari zake kubwa kwa hali ya uhusiano wa kisiasa wa sasa na siku zijazo nchini Kenya.

Lakini je, uamuzi huu hauna makosa? Kuna masuala ambayo yanaweza kudondolewa kutokana na uamuzi huo kuwa yanayoweza kutumiwa katika rufaa?

Iwapo wewe umetuma maombi ya kazi ya jaji na unaulizwa hadharani na jopo linalokuhoji kukosoa uamuzi huo; jibu lako litakuwa nini?

Naam, katika makala haya, nitatoa baadhi ya mambo ya kukosolewa katika uamuzi huo, kwa msimamo wa mwanasheria.

Ukosoaji huu umejengwa kwa msingi kwamba uamuzi huo unaibua masuala mageni; hautoi hali ambayo inafunga jamii ya Wakenya kwa sababu unaweza kubadilishwa au kufutwa na Mahakama ya Rufaa au Mahakama ya Juu.

Kwa hakika, uamuzi huo hautoi kauli ya mwisho hadi Mahakama ya Juu, mamlaka ya upeo zaidi, inayoamua masuala mazito ya kikatiba, itakapotoa uamuzi.

Nitaanza kwa kueleza masuala ya itikadi. Uamuzi wote uko wazi kuhusu kanuni za kimsingi za kufasiri katiba.

Kwa mfano, sehemu kubwa ya uamuzi huo, majaji wamejaribu kwa kina kufafanua maana ya “mpango wa umma” kupitia ufasiri wa katiba lakini wameishia kubuni maeneo makuu yasiyoeleweka.

Linalojitokeza wazi na muhimu kabisa ni kupata kuwa mpango wa umma wa kubadilisha katiba unafaa kutanguliwa na elimu ya jamii, kushirikisha umma kupitia kwa kongamano la wawakilishi.

Hebu nieleze hili linamaanisha nini; hakuna tofauti kuu kati ya elimu ya jamii na kushirikisha umma kwa sababu moja linaweza kutumiwa kuwa lingine.

Ikiwa mkutano umepangwa Mandera kukusanya maoni kuhusu mada fulani ya kushirikishwa katika Mswada, utaratibu unaweza kuwa kusambazwa kwa vijitabu, maelezo kutoka kwa waandalizi wa yaliyomo katika mikutano ya umma na kujumuisha maoni yanayokusanywa kwenye mswada unaoandaliwa.

Utaratibu huu unatimiza elimu ya jamii na kushirikisha umma.

Kwa hivyo, uamuzi kwamba elimu ya jamii na kushirikisha umma hauna utata kwa kuwa Jopokazi la BBI liliandaa mambo haya mawili kwa njia iliyo wazi.

Kongamano la wawakilishi kwa upande mwingine, ni muundo wa kisasa katika sheria ya kikatiba na nadharia lakini ina mizizi katika tabia za Kigiriki/Kiyunani kwamba mamlaka ya mwisho katika serikali ni ya watu.

Martin Loughlin, Mhadhiri wa Sheria ya Umma chuoni London School of Economics anaeleza kuwa mbinu hii inajitokeza kutoka kwa vuguvugu la karne la 18 barani Ulaya la kubadilisha na kuthibitisha lililojulikana kama kuchanua na ina masharti mawili: kutambuliwa kuwa chanzo cha mwisho cha mamlaka ya kisiasa yanatoka kwa watu na kukubali wazo kuwa katiba ni kitu ambacho walitengeneza.

Anaeleza kuwa muundo huu unasimama peke yake tu katiba inapoeleweka kama chombo cha kisheria kinachotoa mamlaka yake katika msingi wa kujitolea: hasa, sasa katiba inadhihirisha nguvu za watu kufanya na kufanya tena mipangilio ya taasisi ambazo wanatawaliwa nazo.

Katika katiba ya Kenya, mbinu ya mamlaka ya kuchagua imetambuliwa katika utangulizi wake. Ibara ya 1 kuhusu uhuru wa watu na misingi katika ibara 10 (ushirikishi wa watu).

Katika muundo wa katiba, watu kwa kawaida hutekeleza mamlaka ya kuchagua kupitia uchaguzi huru na wa haki, kushiriki kikamilifu katika utungaji wa sera na sheria, kupokonya viongozi vita na kura ya maamuzi.

Ili kufanikisha mamlaka haya ya kuchagua, bunge limetunga sheria kama sheria ya uchaguzi kuongoza masuala ya kiutaratibu.

Unavyoeleza uamuzi huo, katiba ya 2010 ilitanguliwa na taratibu na sheria zilizoeleza jinsi shughuli zingetekelezwa.

Lakini inaonekana hakuna sheria kuhusu Ibara ya 257 ya katiba kuhusu mpango wa umma unaohitaji kuitishwa kwa kongamano kama hitaji la lazima.

Zaidi ya hayo, hakuna sheria inayoongoza mpango wa umma. Kile ambacho majaji wamefanya ni kujaza pengo hilo kwa kufafanua na kuwa na kinachofahamika kama “sheria iliyoundwa na jaji” kuhusu suala fulani.

Ikiwa majaji wana nguvu hizo ni jambo lenye utata wa wazi kwamba sababu ya ubishi wa kisheria kuhusiana na mipaka ya kufanya maamuzi na itikadi za utengano wa kimamlaka. (Itaendelea)

Bw Wanyama ni wakili mbobevu

You can share this post!

Usalama waimarishwa Juja tayari kwa uchaguzi mdogo Jumanne

WARUI: Elimu: Serikali itambue mchango wa shule za kibinafsi