• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 5:22 PM
Sossion asema mbinu  ‘chafu’ za TSC kamwe hazitagawanya walimu

Sossion asema mbinu ‘chafu’ za TSC kamwe hazitagawanya walimu

Na Osborne Manyengo

KATIBU Mkuu wa Chama cha Kitaifa cha Walimu (KNUT), Bw Wilson Sossion ameilaumu Tume ya Huduma za Walimu (TSC) kwa kula njama ya kuusambaratisha muungano huo.

Akihutubu wakati wa uchaguzi wa viongozi wa KNUT wa Bonde la Ufa mjini Kitale, Bw Sossion alisema TSC imepokonya KNUT zaidi ya wanachama 200,000. Pia imetishia kuwaachisha kazi walimu wakuu wanaopanga kujiunga na KNUT.

Bw Sossion ameishinikiza wizara ya Fedha kutoa zaidi ya Sh32 bilioni jinsi ilivyopendekezwa na SRC kama nyongeza ya mshahara kwa walimu.

Alisema chama cha KNUT kiko imara na akawataka walimu wasitishwe na yeyote.

“TSC inahujumu utendakazi wa walimu huku ikitumia kila mbinu kusambaratisha chama cha walimu. Inatumia vitisho vya kufuta kazi walimu wakuu. Walianza kuwanyima viongozi wa KNUT mshahara na kupokonya KNUT zaidi ya wanachama laki mbili kwa kuwanunua,” akasema Bw Sossion. Alitangaza kuwa atatetea kiti chake katika uchaguzi mkuu wa kitaifa wa chama hicho mwezi ujao.

 

You can share this post!

Uteuzi wa Kidato cha Kwanza waahirishwa

Jaji Koome atwaa afisi muhimu akiahidi mageuzi