• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
Kafyu kuendelea kwa siku 60 zaidi

Kafyu kuendelea kwa siku 60 zaidi

Na LEONARD ONYANGO

MARUFUKU ya kutokuwa nje kati ya saa 4.00 usiku na saa 10.00 alfajiri itaendelea hadi Julai 27.

Kupitia Gazeti Rasmi la Serikali, Waziri wa Usalama Fred Matiang’i aliongeza muda wa kafyu kwa siku 60.

“Marufuku hii itatekelezwa kati ya saa nne usiku na saa kumi alfajiri kuanzia Mei 28 na itaendelea kwa siku 60.

“Wakati wa masaa ya kafyu, hakutakuwa na mikutano ya umma na safari ya makundi ya watu au mtu mmoja,” akasema Waziri Matiang’i.

Watakaotaka kusafiri wakati wa kafyu watatakiwa kupata idhini ya mkuu wa polisi wa kaunti, kaunti ndogo au kata.

Makundi 27 ya watu wanaofanya kazi katika sekta muhimu kama vile wahudumu wa afya, maafisa wa usalama, wanahabari, wasafirishaji wa mizigo na maafisa wa zimamoto wana sababu maalum.

Wengine ambao hawatazuiliwa kuwa nje wakati wa kafyu ni mafundi wa kutengeneza barabara, madaktari wa mifugo, mawakili wa Mahakama Kuu, maafisa wa Mamalaka ya Ushuru (KRA) na kadhalika.

You can share this post!

Muturi aharibu hesabu ya Raila, Ruto Mlimani

Uhuru aongoza Wakenya kuomboleza Kalembe Ndile