• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
PATA USHAURI WA DKT FLO: Mzio wa chakula huletwa na nini?

PATA USHAURI WA DKT FLO: Mzio wa chakula huletwa na nini?

Mpendwa Daktari,

Mwanangu mwenye umri wa miaka 15 amekuwa na mzio wa maziwa tangu utotoni. Nilidhani tatizo hili lingeisha anavyokua, lakini bado lipo. Mzio wa chakula husababishwa na nini?

Mercy, Mombasa

Mpendwa Mercy,

Mzio wa chakula ni tatizo ambalo hukumba angalau kila mtu wakati mmoja maishani.

Mzio kamili wa chakula ni athari zisizo za kawaida katika mfumo wa kinga mwilini baada ya kula chakula fulani. Watu wanaokumbwa na matatizo haya sharti watambue na kuzuia hasa ikizingatiwa wakati mwingine huwa hatari na hata yaweza sababisha kifo.

Mzio wa chakula hujitokeza vipi?

Allergens kwenye chakula ni viungo ambavyo huchochea mzio mwilini. Kwa wingi viungo hivi huwa protini zinazokataa moto wakati wa upishi, asidi kwenye tumbo na vimeng’enya tumboni. Hivyo hudumu kwenye ukuta wa utumbo, kuingia kwenye mfumo wa damu na kulenga viungo fulani mwilini, na hivyo kusababisha mzio.

Unaweza tokana na matatizo ya kinga mwilini au historia ya matatizo haya katika familia.

Ishara kamili za mzio wa chakula hutokea kati ya dakika kadha au saa moja baada ya kula chakula kinachochochea hali hii. Ishara huanza kama mwasho mdomoni na ugumu wa kumeza chakula au kupumua. Wakati wa mmeng’enyo wa chakula, ishara ambazo hujitokeza ni pamoja na kichefuchefu, kutapika, kuendesha na maumivu ya tumbo.

Mzio mwingi wa chakula hutokea katika kipindi cha mwaka mmoja au miwili ya kwanza. Japo mzio kama maziwa na mayai huisha mtoto anapozidi kukua, kuna mwingine ambao huendelea maishani.

Kwa watoto wachanga, mzio wa chakula hutambuliwa kwa kuchunguza tabia ya mtoto baada ya kubadilisha lishe. Kumnyonyesha mtoto pekee pasipo kumlisha chakula kingine katika miezi minne ya kwanza maishani, husaidia kupunguza uwezekano wa kukumbwa na mzio wa maziwa katika miaka miwili ya kwanza.

Mpendwa Daktari,

Maradhi ya ‘Brittle Bone Disease’ yanatokana na nini?

Johnson, Nairobi

Mpendwa Johnson,

Brittle Bone Disease ni hali ya kuzaliwa nayo inayotokana na mifupa dhaifu ambayo huvunjika kwa urahisi. Hali hii inapotokea hasa huwakumba watoto waliozaliwa katika familia zilizo na historia ya maradhi haya.

Yanaweza kuwa mepesi na kusababisha mifupa kadhaa kuvunjika, au makali na mgonjwa kupoteza uwezo wa kusikia, matatizo ya kupumua, moyo, uti wa mgongo, ubongo na hata kupelekea ulemavu wa kudumu.

Hali hii husababishwa na matatizo ya kijinetiki ambayo huathiri uzalishaji wa type 1 collagen, protini inayotumika kuunda mafupa. Jeni hii hurithiwa lakini kuna wakati mwingine ambapo hutokana na mabadiliko ya ghafla.

Aina za Brittle Bone Disease

•Type 1 OI: Aina hii ni nyepesi zaidi na huwakumba sana watoto wachanga. Hapa, mwili wa mtoto unazalisha kiwango kingi cha collagen lakini hakitoshi.

•Type 2 OI: Aina hii ni hatari sana kwani hata husababisha kifo. Watoto wanaozaliwa na hali hii wanaweza kuwa na kifua chembamba au ubavu uliovunjika au usio wa umbo la kawaida.

•Type 3 OI: Hii husababisha mifupa kuvunjika kwa urahisi hasa pindi baada ya kuzaliwa. Pia yaweza sababisha matatizo ya muundo wa mifupa mtoto anavyozidi kuwa mkubwa.

•Type 4 OI: Aina hii yaweza kuwa nyepesi au kali huku watoto wanaozaliwa wakiwa na miguu iliyojipinda, hali ambayo hata hivyo huimarika na umri.

Ishara za maradhi haya ni pamoja na ulemavu wa mifupa na wakati mwingine kuvunjika, viungo vilivyolegea, kimo kifupi na meno dhaifu, uso kuwa na umbo linalokaribiana na pembe tatu, blue sclera (rangi ya samawati kwenye sehemu nyeupe ya mwili), miguu na mikono iliyojipinda, Kyphosis (uti wa mgongo kujipinda kwa nje), scoliosis (uti wa mgongo kujipinda ubavuni), na kupoteza uwezo wa kusikia, vile vile matatizo ya mfumo wa kupumua na moyo.

You can share this post!

Brazil kuwa mwenyeji wa fainali za Copa America

Wamalwa ahusishwa na chama kipya cha DAP-K kilichosajiliwa