• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 10:06 AM
Beki Eric Garcia abanduka Man-City na kutua Barcelona kwa mkataba wa miaka mitano

Beki Eric Garcia abanduka Man-City na kutua Barcelona kwa mkataba wa miaka mitano

Na MASHIRIKA

BARCELONA watamsajili beki raia wa Uhispania, Eric Garcia kwa mkataba wa miaka mitano baada ya kandarasi yake kutamatika rasmi mwishoni mwa Juni 2021.

Kwa mujibu wa mkataba huo, kikosi chochote kitakachowania huduma za Garcia, 20, kitalazimika kuweka mezani kima cha Sh48 bilioni.

Garcia alianza kupiga soka kitaaluma akivalia jezi za Barcelona nchini Uhispania kabla ya kuyoyomea Uingereza kuvalia jezi za Man-City ugani Etihad mnamo 2017.

Garcia aliyejiunga na Barcelona mnamo 2008, aliwajibikia Man-City mara 12 chini ya kocha Pep Guardiola katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). Hata hivyo, alipangwa katika kikosi cha kwanza mara tatu pekee muhula huu wa 2020-21.

Kwa ujumla, sogora huyo raia wa Uhispania alichezea Man-City mara 35 huku 20 kati ya mechi hizo zikiwa katika msimu wa 2019-20, wakati ambapo alikuwa na uhakika wa kuunga kikosi cha kwanza baada ya Man-City kukabiliwa na visa vingi vya majeraha.

Tangu Septemba 2020, Garcia amechezea timu ya taifa ya Uhispania mara saba na akatiwa kwenye kikosi kitakachotegemewa na kocha Luis Enrique kwenye fainali zijazo za Euro kuanzia Juni 11 hadi Julai 11, 2021.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Vita vya Uhuru na mahakama vingalipo

AFYA: MKU yazindua kituo cha wahadhiri, wanafunzi kufanyia...