• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
Hazina ya NG-CDF kufadhili elimu ya wanafunzi vyuoni

Hazina ya NG-CDF kufadhili elimu ya wanafunzi vyuoni

Na Lawrence Ongaro

WANAFUNZI wa vyuo kutoka Thika wamehimizwa kujikusanya katika makunddi ili wanufaike na fedha za hazina ya kitaifa ya ustawi wa maeneobunge (NG- CDF).

Walishauriwa kuwa wabunifu katika kozi wanazofanya ili watakapokamilisha masomo waanze kujitegemea kwa kujiajiri.

Mbunge wa Thika, Bw Patrick ‘Jungle’ Wainaina, alisema Jumamosi mjini Thika kwamba, tayari Sh4.5 milioni zimetengwa ili kutolewa kwa wanafunzi ambao tayari wako na makundi, kwa lengo la kujiendeleza katika kazi tofauti.

Aliwashauri wanafunzi wanaokamilisha masomo vyuoni kuwa na maono ili wawe waajiri baada ya kujiimarisha kwenye biashara zao.

Aliyasema hayo mnamo Jumamosi mjini Thika katika hafla ya wanafunzi ya maonyesho ya bidhaa tofauti wanazotengeneza na kuzitumia wakiwa vyuoni.

Zaidi ya vyuo 15 vilishiriki kwenye hafla hiyo iliyofana sana.

Baadhi ya vyuo vilivyohudhuria hafla hiyo ni Mount Kenya, Zetech, Cascades, Kenya Institute of Management ( KIM), na Kenya Business and Counseling miongoni mwa vingine.

Baadhi ya kozi zinazoendeshwa kwenye vyuo hivyo ni uokaji wa keki, ushonaji wa nguo, ususi, ujenzi, masomo ya umeme, na mengine mengi.

Wanafunzi wengi waliridhika na mawaidha waliyopokea kutoka kwa washika dau wote waliohudhuria hafla hiyo wakisema watajiunga kwa vikundi ili wanufaike na fedha za maendeleo za NG- CDF.

You can share this post!

Ogallo na Muriu washindia Kenya shaba taekwondo za bara...

Muungano wa kaunti umekufa