• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 8:50 AM
Mkimbizi Msafiri akimbia kilomita zaidi ya kilomita 500 kutoka Nairobi hadi Mombasa kuchangisha fedha za kusaidia wakimbikizi nchini Kenya

Mkimbizi Msafiri akimbia kilomita zaidi ya kilomita 500 kutoka Nairobi hadi Mombasa kuchangisha fedha za kusaidia wakimbikizi nchini Kenya

Na WACHIRA MWANGI

TAFSIRI: GEOFFREY ANENE

Mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amekamilisha mbio za siku tatu kutoka mjini Nairobi hadi Mombasa.

Francois Msafiri, ambaye hushiriki mbio zinazozidi kilomita 42 na pia nyingine ndefu, alikamilisha zaidi ya kilomita 500 akilenga kufanya hamasisho kuhusu hali ya wakimbizi humu nchini.Msafiri anasisitiza kuwa anatumia riadha kuchangisha fedha za kuimarisha elimu bora ya watoto wanaoishi katika kambi za wakimbizi.

Alianza safari yake Juni 4 saa kumi na mbili asubuhi na kufika salama mjini Mombasa dakika chache baada ya sita adhuhuri Jumapili.Anaomba wahisani kusaidia kampeni yake ya kuimarisha maisha ya wakimbikizi.

“Nashiriki mbio hizi ili kuchangishia watoto fedha kuwawezesha kukamilisha masomo yao. Wengi wao wanapata mimba za mapema, wengine wameingilia dawa za kulevya na ninataka kubadilisha mkondo huo mbaya,” alisema Msafiri.

Alifichua kuwa alitumai kukamilisha umbali huo akitumia saa 40, lakini haikuwezekana kwa sababu alichanika msuli kidogo baada ya kilomita ya 300.Meneja wake na kocha Enock Rotich alisema kuwa alifurahia kuwa walifaulu kufika Mombasa.

“Tunafurahi kufika Mombasa baada ya safari ndefu na ya kuchosha. Pongezi kwake. Tunachangisha fedha kusaidia watoto wakimbikizi kielimu na pia kukuza talanta zao. Imekuwa safari ndefu. Tunashukuru maafisa wa usalama katika barabara tuliyotumia kwa kutuelewa licha ya kuwa tuliendelea na safari hata wakati wa kafyu,” alisema Rotich.

Changamoto kubwa, alisema, ilikuwa malori makubwa barabarani yaliyosababisha wapoteze muda.Katibu wa Shirikisho la Riadha Kenya kaunti ya Mombasa, Beatrice Taita alipongeza mwanariadha huyo na kuomba kaunti hiyo itoe mchango wake pamoja na kujenga kambi ya wakimbizi kushughulikia masuala yao.

Afisa anayesimamia michezo katika kaunti ya Mombasa, Innocent Mugabe, aliahidi kuwa kaunti itasaidia kampeni yake na kupongeza juhudi zake za kusaidia watoto.

  • Tags

You can share this post!

Gerrard na Benitez kati ya wakufunzi sita wanaomezea mate...

Ogallo aapa kufukuzia kuwa Mkenya wa kwanza kushiriki Grand...