• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 5:46 PM
Rais wa Ufaransa azabwa kofi na mkazi

Rais wa Ufaransa azabwa kofi na mkazi

Na MASHIRIKA

MWANAMUME mmoja alimzaba kofi Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa alipokuwa akitangamana na raia kusini mwa nchi hiyo jana.

Kwenye video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Macron alinyoosha mkono wake kumsalimia mwanamume aliyekuwa kwenye kundi dogo la watu waliokuwa nyuma ya kizuizi cha chuma.

Kiongozi huyo alikuwa kwenye ziara katika taasisi moja ya mafunzo ya utalii.

Ghafla, mtu aliyekuwa amevalia shati alisema: “Hatukutaki Macron!” Baadaye, alimpiga kofi upande wa kushoto wa uso wake.Hata hivyo, walinzi wa kiongozi huyo walifanikiwa kumkabili mwanamume huyo na kumwezesha kuendelea na shughuli zake.

Kufuatia tukio hilo, watu wawili walikamatwa, kulingana na taarifa za polisi. Asili ya mtu aliyehusika haikubainika mara moja. Macron alikuwa kwenye ziara maalum katika eneo la Drome kukutana na wahudumu wa hoteli na wanafunzi baada ya hali ya kawaida kurejea kutokana na janga la virusi vya corona.

Waziri Mkuu Jean Castex alikashifu vikali kisa hicho, akikitaja kuwa “ukiukaji wa demokrasia.”

 

You can share this post!

Wamaasai waonya Tangatanga dhidi ya kujaribu kupenya Narok

Wakazi kupewa bangi baada kupokea chanjo