• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
Aliyejifungua watoto 10 akiri kushtushwa na mimba yake

Aliyejifungua watoto 10 akiri kushtushwa na mimba yake

Na MASHIRIKA

MWANAMKE aliyejifungua watoto kumi kwa wakati mmoja nchini Afrika Kusini, amesema kuwa alishangazwa na ujauzito wake.

Gosiame Thamana Sitole, 37, alijiufungua watoto hao Jumanne usiku, huku idadi hiyo ikiwa watoto wawili zaidi ya wale aliotarajia kujifungua. Madaktari walikuwa wametabiri kwamba angejifungua watoto wanane.Alijifungua katika hospitali moja jijini Pretoria.

Mumewe, Teboho Tsotetsi alisema kuwa, kutokana na idadi kubwa ya watoto hao, alilazimika kujifungua kupitia njia ya upasuaji.“Nimeshangazwa na ujauzito wangu. Ilikuwa vigumu mwanzoni. Nilikumbwa na maradhi. Ingali vigumu kwangu japo nimezoea.

Sihisi uchungu tena. Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kujifungua kwa njia salama,” akasema.Mwanamke huyo alijifungua wavulana saba na wasichana watatu.Kwenye mahojiano na gazeti la ‘Pretoria News’, alisema mimba yake ilikuwa ya kawaida na hakutumia njia zozote za kisasa.

“Ni wavulana saba na wasichana watatu. Nina furaha na hisia nyingi,” alisema mumewe.Wataalamu wanasema mwanamke huyo amevunja rekodi duniani kwa kuwa mwanadamu wa kwanza kujifungua idadi kubwa zaidi ya watoto.

Awali, rekodi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Halima Cisse kutoka Mali, aliyejifungua watoto saba kwa wakati mmoja nchini Morocco mwezi uliopita.Kabla ya Cisse, rekodi ilikuwa ikishikiliwa na Nadya Suleman kutoka Amerika, aliyejifungua watoto wanane mnamo 2009.

Alijifungua watoto hao kupitia mfumo wa kisasa.?Kwenye mahojiano nyumbani kwake mwezi uliopita, Sitole alisema alishangaa madaktari walipomwambia angejifungua watoto sita baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.Alisema alikaa siku nyingi bila kupata usingizi, akihofia maisha yake binafsi na watoto wake.

“Baadhi ya maswali niliyojiuliza ni ikiwa watoto hao wangetoshea tumboni mwangu. Je, hali ingekuwa vipi ikiwa baadhi yao wangezaliwa wakiwa wameungana? Ni nini kingenifanyikia? Hata hivyo, Mungu alifanya muujiza na nikafanikiwa kujifungua bila tatizo lolote,” akasema.

Kulingana na Prof Dini Mawela, ambaye ndiye naibu wa idara ya masomo ya matibabu katika Chuo Kikuu cha Sefako Makgatho, tukio hilo ni la kipekee.Kutokana na upekee wa tukio hilo, alisema watoto hao watalazimika kuwekwa katika sehemu maalum kwa miezi kadhaa ijayo hadi pale watakapopata nguvu.“Ni tukio la aina yake.

Sifahamu undani wake kuhusu namna lilivyofanyika. Ni mimba yenye upekee mkubwa. Tatizo lililopo ni kwamba, watoto hao hawakuwa na nafasi ya kutosha kwenye tumbo la mama yao. Hilo linawafanya kuwa wadogo sana. Kuna hatari kubwa ikiwa wataanza kulelewa kama kawaida,” akasema.Hadi jana, serikali ya Afrika Kusini haikuwa imetoa taarifa yoyote kuhusiana na tukio hilo la nadra.

  • Tags

You can share this post!

Mshukiwa wa mauaji ya mke aliyekuwa ametoweka anyakwa...

Anaoka keki, mikate mtaani Huruma na ndoto yake ni kuwa na...