Kocha Maurizio Sarri sasa kudhibiti mikoba ya Lazio kwa miaka miwili

Na MASHIRIKA

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO 

LAZIO wamemwajiri kocha Maurizio Sarri kwa mkataba wa miaka miwili.

Ina maana kwamba kocha huyo wa zamani wa Chelsea ambaye pia amewahi kuwa meneja wa benki, atahudumu kambini mwa Lazio hadi Juni 2023.Kwa mujibu wa gazeti la Sportsmail, kubwa zaidi katika maazimio ya Sarri ni kushawishi waajiri wake wapya kujinasia huduma za kiungo mvamizi Ruben Loftus-Cheek wa Chelsea.

Katika msimu wake wa kwanza kambini mwa Chelsea, Sarri aliongoza kikosi hicho kutia kapuni taji la Europa League.Ingawa kwa sasa Loftus-Cheek angali na mkataba na Chelsea hadi 2014, sogora huyo raia wa Uingereza alitumwa kambini mwa Fulham kwa mkopo mnamo 2020-21 baada ya kukosekana katika mipango ya aliyekuwa mkufunzi wa Chelsea, Frank Lampard.

Lazio anarejea katika soka ya Italia wakati ambapo Ligi Kuu ya taifa hilo (Serie A) imeshuhudia mabadiliko mengi katika ngazi ya ukufunzi.Antonio Conte alibanduka ugani San Siro baada ya kushindia Inter Milan ubingwa wa Serie A kwa mara ya kwanza tangu 2009-10. Nafasi yake ilitwaliwa na kocha Simone Inzaghi aliyetokea Lazio.

Aidha, Jose Mourinho aliyetimuliwa na Tottenham Hotspur ametua kambini mwa AS Roma huku Juventus wakimrejesha Massimiliano Allegri kuwa kizibo cha Andrea Pirlo.LAZIO wamemwajiri kocha Maurizio Sarri kwa mkataba wa miaka miwili.

Ina maana kwamba kocha huyo wa zamani wa Chelsea ambaye pia amewahi kuwa meneja wa benki, atahudumu kambini mwa Lazio hadi Juni 2023.Kwa mujibu wa gazeti la Sportsmail, kubwa zaidi katika maazimio ya Sarri ni kushawishi waajiri wake wapya kujinasia huduma za kiungo mvamizi Ruben Loftus-Cheek wa Chelsea.

Katika msimu wake wa kwanza kambini mwa Chelsea, Sarri aliongoza kikosi hicho kutia kapuni taji la Europa League.Ingawa kwa sasa Loftus-Cheek angali na mkataba na Chelsea hadi 2014, sogora huyo raia wa Uingereza alitumwa kambini mwa Fulham kwa mkopo mnamo 2020-21 baada ya kukosekana katika mipango ya aliyekuwa mkufunzi wa Chelsea, Frank Lampard.

Lazio anarejea katika soka ya Italia wakati ambapo Ligi Kuu ya taifa hilo (Serie A) imeshuhudia mabadiliko mengi katika ngazi ya ukufunzi.Antonio Conte alibanduka ugani San Siro baada ya kushindia Inter Milan ubingwa wa Serie A kwa mara ya kwanza tangu 2009-10.

Nafasi yake ilitwaliwa na kocha Simone Inzaghi aliyetokea Lazio.Aidha, Jose Mourinho aliyetimuliwa na Tottenham Hotspur ametua kambini mwa AS Roma huku Juventus wakimrejesha Massimiliano Allegri kuwa kizibo cha Andrea Pirlo.