• Nairobi
  • Last Updated April 16th, 2024 6:55 PM
Loroupe kuongoza timu ya wakimbikizi ya Olimpiki

Loroupe kuongoza timu ya wakimbikizi ya Olimpiki

  Na GEOFFREY ANENE

Mkenya Tegla Loroupe ametajwa kuwa kiongozi wa msafara wa timu ya wakimbizi 29 watakaoshiriki Olimpiki mnamo Julai 23 hadi Agosti 8 mjini Tokyo, Japan.

Kocha Joseph Domongole pia kutoka Kenya amechaguliwa kutia makali timu ya riadha.Wanariadha wanne wanaoishi na kufanya mazoezi katika kituo cha amani cha Tegla Loroupe katika eneo la Ngong, wako katika kikosi hicho.

Kilidhinishwa na na kuzinduliwa na bodi ya viongozi wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC).Wanariadha kutoka kituo cha Loroupe kikosini ni wakimbiaji Rose Nathike Lokonyen (mita 800), James Nyang Chiengjiek (mita 800), Angelina Nadai Lohalith (mita 1500) na Paulo Amotun Lokorio (mita 1500).

Kamati ya Kitaifa ya Olimpiki Kenya (NOC-K) kupitia kwa rais wake Paul Tergat, imepongeza timu hiyo kutoka kituo cha Kenya pamoja na kutajwa kwa Loroupe kuwa tena kiongozi wa timu hiyo ya wakimbikizi.

Wakimbikizi hao 29 wanashiriki michezo mbalimbali. Wanatoka katika mataifa 13 tofauti wanakoishi. Watakuwa sehemu ya timu ya Olimpiki ya wakimbikizi maarufu EOR. Watakuwa wa pili kuingia uwanjani mjini Tokyo baada ya Ugiriki.

Sherehe ya kuzindua kikosi hicho iliendeshwa na rais wa IOC Thomas Bach. Ilihudhuriwa na kamishna wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) Filippo Grandi.Timu ya wakimbikizi ni ya kwanza kutajwa rasmi.

Itashiriki riadha, ndondi, badminton, upigaji wa makasia, uendeshaji baiskeli, karate, ulengaji shabaha kwa kutumia bunduki, miereka na judo.Inajumuisha pia wanamichezo sita walioshiriki Olimpiki 2016 mjini Rio de Janeiro nchini Brazil ambao ni Yusra Mardini (muogeleaji), Popole Misenga (judo) na wakimbiaji James Nyang Chiengjiek (mita 800), Angelina Nadail Lohalith (mita 1500), Paulo Amolin Lokoro (mita 1500) na Rose Nathike Likonyen (mita 800).

You can share this post!

Kocha Maurizio Sarri sasa kudhibiti mikoba ya Lazio kwa...

Bajeti 2021/2022: NMS yakumbukwa