Bajeti 2021/2022: Walioathirika na corona watengewa Sh23.1 bilioni

Na SAMMY WAWERU

SERIKALI imetangaza itaendeleza mpango wa kusaidia walioathirika kufuatia athari za virusi vya corona.

Kenya ilithibitisha kuwa mwenyeji wa janga la Covid-19 Machi 2021, na maelfu na mamilioni ya watu walipoteza ajira.Wengine, biashara zao zilifisika na kufungwa.Katika Makadirio ya Bajeti Mwaka wa Fedha 2021/2022, serikali imesema imetenga mgao wa Sh23.1 bilioni kupiga jeki wanaohangaika, kutokana na athari za corona.

“Serikali pia imetenga mgao wa Sh3 bilioni kuendeleza mpango wa Kazi Mtaani,” akasema Waziri wa Fedha, Bw Ukur Yattani wakati akisoma makadirio hayo ya matumizi ya fedha za serikali kuu.Mradi wa Kazi Mtaani ulizinduliwa mwaka uliopita, na Rais Uhuru Kenyatta, ukilenga vijana wasio na kazi na waliopoteza ajira kufuatia corona.

Aidha, unahusisha usafi wa mazingira.Katika makadirio hayo ya bajeti, Bw Yattani pia alisema sekta ya mazingira imetengewa mgao wa Sh6.9 bilioni.Makadirio ya Bajeti Mwaka wa Fedha 2021/2022, ni ya Sh3.66 trilioni.