• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 1:47 PM
FKF yafanikisha klabu 11 za Nairobi kupokea chanjo ya pili ya AstraZeneca

FKF yafanikisha klabu 11 za Nairobi kupokea chanjo ya pili ya AstraZeneca

Na GEOFFREY ANENE

KLABU 11 zinazoshiriki Ligi Kuu nchini na kutoka katika kaunti ya Nairobi, zimepokea chanjo ya pili ya Covid-19 katika ukumbi wa kimataifa wa Kasarani mnamo Ijumaa.

Zoezi hilo lilifanikishwa na Shirikisho la Soka Kenya (FKF) kwa ushirikiano na Wizara za Michezo na Afya.Klabu za kwanza kupokea chanjo hiyo ya AstraZeneca ni Wazito na Bidco United saa tatu asubuhi.Mabingwa wa ligi wa msimu uliopita, Gor Mahia pamoja na Kariobangi Sharks walikuwa wa pili saa moja baadaye.

Gor na Sharks walipokea chanjo hiyo siku moja tu baada ya kuonana uso kwa macho katika mechi ya robo-fainali ya FKF Betway Cup ugani Utalii. Vijana wa kocha Vaz Pinto walinyuka Sharks 2-0 na kutinga nusu-fainali ya kipute hicho cha kutafuta mwakilishi wa Kenya katika Kombe la Mashirikisho la Afrika (CAF).

Vikosi vya KCB na Mathare United vilichanjwa saa tano halafu Nairobi City Stars na Posta Rangers wakapokea chanjo zao saa sita adhuhuri.Sofapaka na viongozi wa Ligi Kuu ya msimu huu wa 2020-2021 Tusker walipata chanjo saa saba mchana kabla ya AFC Leopards kuwa ya mwisho kufunga siku saa nane alasiri.

Klabu zinazopatikana nje ya Nairobi ni Bandari kutoka kaunti ya Mombasa, Kakamega Homeboyz (Kakamega), Nzoia Sugar (Bungoma), Ulinzi Stars (Kericho), Western Stima (Kisumu) na Vihiga United (Vihiga).

  • Tags

You can share this post!

Spika ataka Yatani akamatwe kwa kukaidi seneti

Chepng’etich aweka rekodi mpya ya Kenya ya mita 1,500...