• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 8:55 AM
Jumba llililoanza kujengwa enzi za Moi latengewa bajeti ya Sh500 milioni

Jumba llililoanza kujengwa enzi za Moi latengewa bajeti ya Sh500 milioni

Na SAMWEL OWINO

Jengo lililoanza kujengwa wakati wa utawala wa Hayati Daniel arap Moi limetengewa Sh500 milioni katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2021/2022 iliyosomwa Alhamisi na waziri wa Fedha Ukur Yattani.

Jengo hilo la Makao Makuu ya Baraza la Mtihani (Knec, maarufu kama Jumba la Mtihani, lilianza kujengwa miaka 33 iliyopita na kufikia sasa halijakamilika.Katika bajeti ya mwaka uliopita wa fedha (2019/2020), jumba hilo pia lilitengewa Sh395 milioni.

Wabunge wameonya kuwa watawachukulia hatua wahusika iwapo jumba hilo halitakamilika mwaka huu.Kamati ya Bunge kuhusu Elimu, sasa inashutumu baadhi ya maafisa serikalini kwa kujinufaisha wao binafsi kutokana na mradi huo kila mwaka.

Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu katika Bunge la Kitaifa Florence Mutua aliambia Taifa Jumapili kuwa kuna baadhi ya watu katika baraza la Knec ambao wamekuwa wakinufaika na mradi huo.“Ni aibu kwamba kujikokota kwa mradi huo ni sherehe kwa baadhi ya maafisa Knec.

“Jumba hilo ni sharti likamilike mwaka huu ili liokoe Sh110 milioni za walipa ushuru ambazo baraza la Knec limekuwa likilipa kodi ya nyumba kila mwaka ,” akasema Bi Mutua bila kuwataja.Mbunge wa Kisauni Ali Mbogo alihoji ni kwa nini jumba la Mtihani limekuwa likitengewa fedha kila mwaka lakini halijawahi kukamilika.

“Miaka 33 ni muda mrefu sana. Jumba hilo lilifaa kukamilika miaka mingi iliyopita. Bunge linafaa kuwachukulia hatua wahusika kwani fedha zinazotumika ni za walipa ushuru,” akasema Bw Mbogo.Kamati ya Bunge kuhusu Bajeti imeonya wizara za serikali dhidi ya kuanzisha miradi mipya kabla ya kukamilisha iliyopo.

Kamati hiyo inayoongozwa na mbunge wa Kieni Kanini Kega imeonya kuwa wizara itakayoanzisha miradi mipya kabla ya kukamilisha iliyoko, itapunguziwa bajeti.Lengo la kujenga jumba la Mtihani ilikuwa kuhakikisha kuwa shughuli zote za Knec zinafanyika ndani ya jengo moja katika mtaa wa South C, karibu na Barabara ya Mombasa jijini Nairobi.

Mradi huo unajumuisha ujenzi wa majengo matatu A, B na C yaliyo na ghorofa sita kila moja.

  • Tags

You can share this post!

Magavana tumbototo kuhusu miradi waliyoanza

Ngarambe ya Copa America yang’oa nanga usiku wa leo