• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 6:21 PM
Njia asili ya kuondoa visunzua yaani warts

Njia asili ya kuondoa visunzua yaani warts

Na MARGARET MAINA

[email protected]

VISUNZUA ni warts kwa Kiingereza. Hivi ni vinyama vinavyoota kwenye ngozi ambavyo husababishwa mara nyingi na maambukizi.

Matatizo ya ngozi hutofautiana sana kuanzia kwa dalili na athari ikiwemo ukali. Baadhi huwa ya muda au ya kudumu ilhali mengine hutoweka baada ya muda mchache.

Visunzua ni vinyama vinavyoota juu ya ngozi ambapo vinaweza kutokea usoni, kuzunguka jicho, shingo, mgongoni na kadhalika.

Visunzua au vinyama vyeusi husababishwa na matatizo ya homoni wakati wa ujauzito au unene kupita kiasi.

Matibabu yake hufanyika hospitalini ambapo vinatolewa na vifaa maalumu.

Pia unaweza kuvitibu nyumbani kwa njia za asili.

Kitunguu saumu

Kiponde alafu paka maji yake juu ya kisunzua. Njia hii inaondoa haraka kisunzua ila inauma. Pia jitahidi maji ya kitunguu saumu yasiguse ngozi kwani yanaunguza.

Paka mara mbili kwa siku.

Kiazi mviringo

Kioshe kiazi halafu kikate kiwe vipande vidogo kisha paka maji yake juu ya kisunzua. Sugua kwa kutumia kipande cha kiazi.

Kitunguu maji

Kikate halafu sugua juu ya kisunzua.

Limau

Kata limau kisha sugua juu ya kisunzua likiwa na maji.

Uzi

Kama kisunzia ni kikubwa unaweza kutumia uzi. Loweka uzi kwenye maji ya limau au kitunguu, kisha kifunge mara kwa mara.

Njia nyingine ni rangi ya kucha, siki ya apple cider na ganda la ndizi mbivu.

Njia zote hizi, tumia mara mbili kwa siku. Unaweza kuona kama havitoki ila baada ya mwezi vitaondoka.

You can share this post!

Familia yahangaika baada ya kupata mwili uliokuwa umetoweka...

Shule mpya ya msingi ya Mutuya yafunguliwa Ruiru