• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 8:55 PM
Itakuwa moto Italia, Ubelgiji zikikwaruzana robo ya Euro hii leo

Itakuwa moto Italia, Ubelgiji zikikwaruzana robo ya Euro hii leo

Na MASHIRIKA

MUNICH, Ujerumani

ITALIA na Uhispania watalenga kuendeleza rekodi zao nzuri dhidi ya Ubelgiji na Uswisi mtawalia, dimba la Euro 2020 litakapoingia robo-fainali hii leo Ijumaa.

Azzurri walipepeta mashetani wekundu wa Ubelgiji 2-0 mara ya mwisho walikutana kwenye kombe hili mwaka 2016.

Kwa jumla, Italia imezaba Ubelgiji mara nne, kutoka sare mbili na kupoteza mechi tatu tangu 1954.

Leo, vijana wa Roberto Mancini watajibwaga uwanjani Allianz Arena wakiwa na motisha ya kutopoteza michuano 31 mfululizo, baada ya kuchabanga Austria 2-1 na kujikatia tiketi ya robo-fainali.

Wanafukuzia ushindi wao wa 13 mfululizo, ingawa wanatarajiwa kupimwa vilivyo ukatili wao dhidi ya Ubelgiji, ambayo haijapigwa katika michuano 13.

Ubelgiji ya kocha Roberton Martinez inatafuta ushindi wake wa sita mfululizo.

Uhispania nayo imepoteza mara moja, kutoka sare tatu na kulisha Uswizi vichapo vinne.

Uswizi, ambayo itakuwa bila nyota Granit Xhaka kutokana na adhabu ya kadi za njano, itamtegemea Haris Seferovic huku Uhispania ikijivunia kinda matata Ferran Torres.

Iliduwaza Ureno anayochezea gunge Cristiano Ronaldo 1-0 katika raundi ya 16-bora lililofungwa na Thorgan Hazard.

Kuhusu vikosi ni kuwa Italia huenda ikakosa beki Giorgio Chiellini aliyechanika misuli nayo Ubelgiji inakodolea macho kuwa bila viungo matata Kevin De Bruyne na Eden Hazard. Wako na majeraha.

Macho yatakuwa kwa wachezaji Thorgan na mshambuliaji wa Italia, Ciro Immobile.

Uhispania nayo imepoteza mara moja, kutoka sare tatu na kulisha Uswizi vichapo vinne.

Uswizi, ambayo itakuwa bila nyota Granit Xhaka kutokana na adhabu ya kadi za njano, itamtegemea Haris Seferovic huku Uhispania ikijivunia kinda matata Ferran Torres.

You can share this post!

Usawa Kwa Wote Party chaendelea kusajili wanachama wake

Ryan Bertrand sasa ni mali rasmi ya Leicester City baada ya...