• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 12:26 PM
Viongozi wa Kiislamu washutumu TSC kutoajiri walimu wengi wa IRE

Viongozi wa Kiislamu washutumu TSC kutoajiri walimu wengi wa IRE

Na FARHIYA HUSSEIN

VIONGOZI wa dini ya Kiislamu kutoka Pwani wameikashifu Tume ya Kuajiri Walimu (TSC) kwa kutoa nafasi chache za walimu wa somo la dini hiyo (IRE).

Viongozi hao wamelalamika kuwa hali hiyo inazidi kusababisha uhaba wa walimu wa somo hilo hasa katika shule za umma na wakaipa TSC saa 72 kuongeza nafasi za walimu hao katika mpango wa kuajiri walimu.

“Kati ya nafasi zilizotolewa za kufundisha nchini na TSC, 12 tu ndio zimeeza kupeanwa kwa walimu wa IRE. Hiyo si haki,” alisema Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Waislamu wa Kenya (Kemnac), Sheikh Juma Ngao.

Aliongeza kuwa wengi wa walimu hao hawana kazi na hulazimika kufunza masomo nyumbani ilhali wengi wao wamehitimu chuo kikuu.

“Tuna vyuo vikuu vya Kiislamu karibu kila eneo la nchi, lakini walimu hawa wanapohitimu huwa hawana mahali pa kufundisha,” alisema Sheikh Ngao.

You can share this post!

Ryan Bertrand sasa ni mali rasmi ya Leicester City baada ya...

Baada ya sare na Gor Mahia sasa Bandari FC yapania kuichapa...