• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
Cha kufanya ili uwe na uso laini na unaong’aa

Cha kufanya ili uwe na uso laini na unaong’aa

Na MARGARET MAINA

[email protected]

ILI uwe na ngozi nzuri yenye kuvutia, unahitaji uvumilivu na uratibu wa mpangilio fulani.

Si swala la siku moja.

Huu hapa ni utaratibu wa kukuelekeza ili uwe na ngozi inayovutia.

Maji

Anza siku yako kwa glasi ya maji fufutende yenye slesi kadhaa ya limau ndani yake.

Hakikisha unakunywa si chini ya glesi nne za maji kwa siku.

Maji husaidia ngozi kuwa na afya na yenye kuvutia.

Unywaji maji ya kutosha unafanya ngozi yako iwe na rutuba na kuondoa mikunjo.

Kujipenda

Unachojisikia ndani ya moyo wako ndicho ambacho kitatoka nje. Ukiwa na msongo wa mawazo kwa kujijadili kuhusu mwonekano wako, kuna uwezekano kwamba ngozi yako itaharibika. Hakikisha unajisifu kila siku kwa kuwa na mawazo chanya zaidi maishani.

Utunzaji wa ngozi

Unahitaji kuijali ngozi yako kwa kununua vipodozi vinavyoendana na ngozi yako. Pia kula vyakula vinavyorutubisha ngozi yako. Vile vile ni muhimu upake sun screen kuikinga ngozi dhidi ya miale hatari ya jua na kuwa na mpangilio wa kuitunza ngozi yako.

Usingizi wa kutosha

Hakikisha unalala kwa muda wa saa nane (8) si chini ya mara nne kwa wiki.

Faida za kupata usingizi wa kutosha

  • hupunguza mikunjo katika ngozi
  • ngozi hujikarabati yenyewe usiku
  • vipodozi vyako au mafuta uyatumiayo kwa ngozi yako hupata muda wa kutosha kufanya kazi

You can share this post!

Ford Kenya yakanusha kufanya mazungumzo ya 2022 na Dkt Ruto

Cristiano Ronaldo aibuka Mfungaji Bora wa Uefa Euro 2020