• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 2:16 PM
Kampeni ya kugawa Huduma Namba yaanza

Kampeni ya kugawa Huduma Namba yaanza

Na KENYA NEWS AGENCY

KAMPENI ya nyumba hadi nyumba imeanzishwa katika kaunti ya Garissa kwa ajili ya kusaka wenye kadi 9,000 za Huduma Namba ambazo hazijachukuliwa.

Kampeni hiyo inaendeshwa na machifu na manaibu wao kufuatia agizo la Kamishna wa kaunti hiyo Boaz Cherutich.

Kulingana Bw Cherutich, ukame na uharibifu wa mitambo ya kurusha mawimbi ya mawasiliano unaofanywa na al-Shabaab umekatiza mawasiliano ya simu, hali ambazo zimechangia mrundiko wa kadi hizo.

Kufikia sasa zaidi ya kadi 9,938 kati ya 22,996 zilizofikishwa Garissa hazijachukuliwa na wenyewe.

“Wakazi wengi aidha wamehamia maeneo mengine kusaka maji na lishe au hawajapokea jumbe fupi za kuwaelekeza mahala pa kuchukua kadi zao. Hii ni kutokana na matatizo ya mawasiliano ya simu eneo hili,” akaeleza Bw Cherutich.

You can share this post!

Mashindano ya kuogelea sasa kuanza Ijumaa jijini Mombasa

Muturi awarai vijana wasake vyeo vya uongozi