• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 12:45 AM
AKILIMALI: Ndege wa mapambo wanavyompa tonge nono mwalimu huyu

AKILIMALI: Ndege wa mapambo wanavyompa tonge nono mwalimu huyu

Na PAULINE ONGAJI

LICHA ya kuwa amesomea ualimu, Bw Paul Wanjohi, 25, amebobea katika masuala ya ufugaji ndege.

Lakini ufugaji wake sio ule wa kawaida kwani ndege anaowafuga sio wa kawaida. Bw Wanjohi anafuga ndege wa mapambo, shughuli anayoiendesha katika kijiji cha Karindundu, Mathira, Kaunti ya Nyeri.

“Mbali na kufuga ndege wa chakula kama vile kuku, bata na bata mzinga, pia nafuga ndege kama vile kanga, Indian runner ducks, Rouen ducks, Swedish blue ducks, Khaki Campbell ducks, Silkie bantam chicken, bearded bantam chicken, booted bantam chicken, fantail pigeons na njiwa, miongoni mwa wengine,” aeleza.

Miaka minne baada ya kuanzisha mradi huu, anamiliki ndege 50 na vifaranga 20, wanaomletea kipato cha kati ya Sh 25,000 na Sh 30,000 kila mwezi.

“Ndege wanaoniletea kipato kikubwa ni bata mzinga na Silkie bantams. Hii ni kwa sababu wanataga mayai mengi wakilinganishwa na kwa mfano, kuku wa kienyeji,” aongeza.

Idadi kubwa ya wateja wake ni majirani wake, lakini pia bidhaa zake zinafika sehemu zingine nchini ambapo yeye hupata wateja wake kupitia mtandao wa kijamii; ukurasa wake wa mtandao wa Facebook: Paul’s Turkey farm Karatina.

“Pia, niko katika vikundi mbalimbali vya WhatsApp ambapio mimi hutangaza bidhaa zangu,” aongeza.

You can share this post!

Eliud Kipchoge alenga kufanya kitu atakachokumbukwa nacho...

AKILIMALI: Jinsi vijana watatu Mathare Kaskazini...