• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
Jinsi ya kuandaa meatballs

Jinsi ya kuandaa meatballs

Na MARGARET MAINA

[email protected]

MEATBALLS ni nyama ambazo zimepikwa na huwa na umbo la mpira.

Meatballs ni aina ya chakula ambacho kinaweza kuliwa na mtu yeyote.

Muda wa kuandaa: Dakika 20

Muda wa mapishi: Dakika 10

Walaji: 4

Vinavyohitajika

  • nyama iliyosagwa kilo 1
  • mazenga (Breadcrumbs)
  • kitunguu maji na kitunguu saumu
  • mayai
  • pilipili kwa apendaye
  • mkate
  • mafuta ya kupikia

Maelekezo

Chukua nyama iliyosagwa kiasi unachopenda.

Loweka angalau slesi mbili za mkate kwenye maji kidogo.

Changanya nyama iliyosagwa na slesi za mkate zilizolowekwa kidogo kwenye maji ili zishikane na nyama.

Katakata viungo ulivyoviandaa; kitunguu maji na kitunguu saumu.

Koroga mayai uliyoyaandaa.

Unganisha meatballs kwa kutumia mikono yako; yaani ziwe na umbo la mpira.

Weka meatballs zako kwenye mayai uliyokoroga.

Toe meatballs ukiziweke kwenye mazenga (Breadcrumbs)

Sasa anza kukaanga meatballs zako kwa kuzitumbukiza kwenye mafuta yaliyochemka katika chombo safi na subiri hadi zigeuke ziwe na rangi ya hudhurungi ndipo uzitoe.

Toa kwenye mafuta na ziweke mahali tayari kwa kula.

Waweza kupakua kwa wali, pasta au chochote ukipendacho.

You can share this post!

Wagombea wa UDA, Jubilee eneobunge la Kiambaa wawarai...

Je, IEBC yafaa kuanza kujiandaa kwa kura ya maamuzi kabla...