• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
Kinara wa upinzani Tanzania akabiliwa na kesi ya ugaidi

Kinara wa upinzani Tanzania akabiliwa na kesi ya ugaidi

Baada ya kumzuilia kwa takribani siku mbili, polisi walisema kwamba kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe anakabiliwa na tuhuma mbalimbali ikiwemo za kupanga njama za kufanya vitendo vya kigaidi na kuua viongozi wa Serikali.

Taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime ilisema, bila kutoa maelezo zaidi, kwamba kumekuwa na upotoshaji mkubwa kwamba Mbowe alikamatwa kwa tuhuma za kupanga na kuandaa kongamano la Katiba mpya jijini Mwanza, jambo ambalo si kweli.

“Mbowe alikuwa anafahamu fika kuwa tuhuma zinazomkabili zilikuwa zinachunguzwa na wakati wowote angehitajika na polisi kwa hatua za kisheria mara tu uchunguzi wake utakapokamilika.

Hatua hiyo imefikiwa sasa,” alisema Misime.Misime alisema kwamba Mbowe hakukakamatwa kwa sababu ya kuandaa mkutano wa katiba mpya mbali alitaka kutumia mkutano huo kupotosha umma kuhusu kukamatwa kwake.

Chadema kilisema kwamba polisi walifanya msako katika nyumba ya Mbowe jijini Dar es Salaam na kutwaa laptopu yake na vifaa vingine kutoka kwa watu wa familia yake kabla ya kumhamishia kituo cha polisi cha Central jijini humo.

“Tulipokea habari za kushtusha kwamba Mbowe atashtakiwa pamoja na watu wengine kwa ugaidi,” chama kilisema kwenye taarifa kupitia Twitter.Mbowe na maafisa wengine wa Chadema walikamatwa wakiwa jiji la Mwanza kabla ya mkutano wa kushinikiza mageuzi ya katiba nchini Tanzania.

Mkuu wa polisi wa eneo hilo Ramadhan Ngh’anzi alisema kwamba Mbowe atarejeshwa Mwanza kuungana na washukiwa wengine waliokamatwa kwa kuandaa mkutano uliopigwa marufuku.

“Kwa sasa yuko salama katika kituo cha polisi cha Central jijini Dar es Salaam,” aliambia wanahabari.Kukamatwa kwake kulijiri miezi minne baada ya Rais wa kwanza mwanamke wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuingia mamlakani kufuatia kifo cha ghafla za John Magufuli, ambaye utawala wake ulilaumiwa kwa kukadamiza upinzani.

Mnamo Aprili, Hassan aliahidi upinzani kwamba angetetea demokrasia na haki za kimsingi.Kulikuwa na matumaini makubwa kwamba kungekuwa na mabadiliko Tanzania baada ya utawala wa Magufuli.Hata hivyo, kukamatwa kwa viongozi wa Chadema kumelaaniwa na makundi ya kutetea haki na wanaharakati wa upinzani wakisema ni thibitisho serikali ya Hassan haivumilii wanaoipinga.

Shirika la Amnesty International lilitaja kukamatwa kwa Mbowe na viongozi wa upinzani kama tisho kwa uthabiti ambao nchi hiyo imekuwa ikijivunia eneo hili.

“Serikali ya Tanzania ni lazima ikome kulenga upinzani na kujaribu kufifisha demokrasia,” alisema Flavia Mwangovya, naibu mkurugenzi wa Amnesty International Afrika Mashariki.Ilisema kwamba kukamatwa kwa viongozi wa upinzani Tanzania ni upuuzaji wa utawala wa sheria na haki za binadamu ikiwemo haki za kujieleza na kukusanyika.

Kukamatwa huku kunakochochewa kisiasa kunafaa kukomeshwa,” ilisema taarifa ya shirika hilo.Amerika ilisema itathibitisha maelezo kuhusu kukamatwa kwa Mbowe lakini ikasema kunazua wasiwasi.

  • Tags

You can share this post!

WANDERI KAMAU: Rais Samia amevunja ahadi yake kurejesha...

Rais abadilisha simu baada ya jaribio la wadukuzi dhidi yake