• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 12:32 PM
Wauzaji pombe Nakuru waonywa

Wauzaji pombe Nakuru waonywa

NA RICHARD MAOSI

GAVANA wa Nakuru Lee Kinyanjui ametoa onyo kali kwa wanaoendesha biashara ya pombe haramu kuanzia Molo, Elburgon, Subukia na Lanet.

Akizungumza na Taifa Leo siku ya Ijumaa alisema kuwa ni hali ambayo imechangia utovu wa maadili katika jamii.

“Inasikitika kuona wanawake na watoto wakihangaika nyumbani kwa sababu waume wanashindwa kutekeleza majukumu muhimu ya kifamilia,”akasema.

Aliwaonya wanaume dhidi ya kubugia pombe kupita kiasi, ikizingatiwa kuwa madhara yake ni makubwa kijamii na hakuna mtu ambaye aliwahi kufariki kutokana na kuacha pombe.

Alisema kuwa pombe haramu ina madhara mengi yakiwemo kupofuka na vifo.

Alidokeza kuwa atashirikisha sekta ya kudhibiti vileo, ili kuhakikisha wagema wana leseni za kuendesha biashara ya pombe.

Aidha alieleza kuwa kaunti itaweka mikakati ya kuwafundisha watengenezaji wa pombe za kienyeji namna ya kuandaa vileo safi na salama kwa matumizi ya binadamu mojawapo ikiwa ni Busaa.

Hili linajiri raia raia wakienelea kulaumu idara ya usalama, kwa kushirikiamna na wauzaji pombe ambapo kila mwezi polisi huchukua hongo na kuwaacha waendelee na biashara.

Baadhi yao wamekuwa wakishinikiza maafisa wa usalama kushirikiana na wazee wa nyumba kumi ili kuhakikisha kuwa matumiza ya pombe haramu yanatokomezwa mara moja.

Mitaa ya mabanda ya Kivumbini, Rhonda, Mwariki na Kapkures yanaongoza kwa idadi kubwa ya wafanyibiashara wanaotengeneza pombe haramu ili kujikimu kimaisha.

  • Tags

You can share this post!

Kamishna apiga marufuku wakazi kula matangani

Mwitaliano ashtakiwa kuiba teksi