• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 8:50 AM
Vyombo vya habari vyahimizwa visaidie NLC kuangazia masuala ya ardhi

Vyombo vya habari vyahimizwa visaidie NLC kuangazia masuala ya ardhi

Na SAMMY WAWERU

TUME ya Kitaifa ya Ardhi (NLC) imevihimiza vyombo vya habari kuisaidia katika uangaziaji wa masuala ya ardhi na mashamba nchini.

Taasisi hiyo ya kiserikali iliyotwikwa jukumu la kuangazia mizozo ya ardhi ya wananchi na umma, imesema ushirikiano wake na vyombo vya habari utasaidia kwa kiasi kikubwa kuangazia mizozo ya ardhi.

“Wanahabari na mashirika wanayofanyia kazi wawe huru kuwasiliana na NLC kwa kisa chochote kile cha mzozo wa ardhi,” akahimiza Afisa Mkuu Mtendaji wa NLC, Bi Kabale Tache.

“Vyombo vya habari vishirikiane nasi kuangazia mizozo ya ardhi na mashamba nchini,” akaongeza.

Afisa huyo alisema visa vya mizozo vinavyoshuhudiwa vitaweza kuangaziwa na kupata suluhu, asasi za habari zikijituma kuvifichua.

NLC ilibuniwa ili kusaidia umma kupata haki ya mashamba.

Hata hivyo, baadhi ya maafisa wake wamekuwa wakituhumiwa kushirikiana na wahuni wanyakuzi wa ardhi.

You can share this post!

Benki ya Equity yafadhili wanafunzi 167 Kiambu

Chepng’etich kufunga safari ya kuenda Japan kutetea...