• Nairobi
  • Last Updated April 16th, 2024 7:55 AM
Barcelona na Neymar waafikiana kusuluhisha mzozo wa kifedha nje ya korti

Barcelona na Neymar waafikiana kusuluhisha mzozo wa kifedha nje ya korti

Na MASHIRIKA

BARCELONA wameafikiana na mshambuliaji Neymar Jr kusuluhisha mzozo wa kifedha kati yao nje ya mahakama.

Neymar ambaye ni fowadi raia wa Brazil mwenye umri wa miaka 29 aliwahi kudai kwamba Barcelona walikataa kumlipa bonasi za Sh5.8 bilioni alipokamilisha uhamisho wake wa Sh26 bilioni hadi Paris Saint-Germain (PSG) ya Ufaransa mnamo 2017.

Badala yake, Barcelona walifika mahakamani kumshtaki Neymar huku wakidai Sh1.2 bilioni ambazo sogora huyo alipokezwa baada ya kutia saini mkataba mpya nao mnamo 2016.

Mbali na fedha hizo, Neymar pia alitakiwa kulipia gharama zote nyinginezo ambazo zilitolewa na Barcelona wakati wa mchakato huo wa kisheria.

Mnamo Juni 2020, mahakama kuu ya Uhispania iliamuru Neymar kufidia Barcelona kima cha Sh951 milioni.

Hata hivyo, fowadi huyo alikata rufaa dhidi ya maamuzi hayo ya korti na kuishtaki upya Barcelona ambayo kwa sasa imethibitisha kwamba wamekutana na Neymar na kupata suluhu ya kudumu nje ya mahakama.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

SHINA LA UHAI: Huduma mbovu katika hospitali za Kaunti...

Jinsi ya kuandaa katlesi za kuku