• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 3:53 PM
Rashford ataka fedha zilizochangishwa na mashabiki kukarabati mnara wake zitumiwe kununulia wanafunzi chakula nchini Uingereza

Rashford ataka fedha zilizochangishwa na mashabiki kukarabati mnara wake zitumiwe kununulia wanafunzi chakula nchini Uingereza

Na MASHIRIKA

MAMILIONI ya pesa zilizochangishwa na mashabiki mtandaoni baada ya mnara wa fowadi Marcus Rashford wa Manchester United kuvunjwa sasa zitatolewa kama msaada kwa ajili ya chakula cha wanafunzi kutoka familia zisizojiweza nchini Uingereza.

Mnara huo wa Rashford uliharibiwa na mashabiki wenye hasira baada ya Uingereza kupigwa na Italia kwenye fainali ya Euro 2020.

Rashford, Bukayo Saka wa Arsenal na Jadon Sancho ambaye sasa amesajiliwa na Man-United kutoka Borussia Dortmund walipoteza penalti zao na kuwapa Italia ushindi wa 3-2 kwenye fainali hiyo iliyochezewa ugani Wembley, London.

Ingawa hivyo, mashabiki sugu wa Rashford walichangisha kima cha Sh6.2 milioni mtandaoni huku wakiandika jumbe za kutia moyo kwenye mnara wake katika eneo la Withington na kukashifu ubaguzi wa rangi miongoni mwa wanasoka.

Rashford sasa ametaka fedha hizo kutolewa kama msaada kwa kituo cha watoto cha Fare Share Greater Manchester.

Fedha nyinginezo zitakazochangishwa na mashabiki kuanzia sasa zitaelekezwa katika shughuli za kuukarabati mnamo wa Rashford ambaye amekuwa mstari wa mbele kuwapa wanafunzi chakula tangu janga la corona litue nchini Uingereza.

Mnara wa Rashford umejengwa katika Barabara Kuu ya Copson ambapo Rashford alilelewa na kuanzia masomo.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Jinsi ya kuandaa katlesi za kuku

Wafugaji na wafanyabiashara wahimizwa kutathmini namna ya...