• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 5:46 PM
Bermuda yawa nchi ya kwanza ndogo zaidi kuwahi kuzoa medali ya dhahabu kwenye Olimpiki

Bermuda yawa nchi ya kwanza ndogo zaidi kuwahi kuzoa medali ya dhahabu kwenye Olimpiki

Na MASHIRIKA

IKIWA na idadi ya watu 63,000 pekee, Bermuda iliweka historia kwa kuwa taifa la kwanza ambalo ni dogo zaidi kuwahi kuzoa dhahabu ya Olimpiki baada ya Flora Duffy kutawala mashindano ya triathlon jijini Tokyo, Japan.

Duffy, 33, alikuwa akinogesha mashindano ya Olimpiki kwa mara ya nne. Aliwapiku wapinzani wengine 55 baada ya kusajili muda wa saa 1:55.36 na kuacha Georgia Taylor-Brown wa Uingereza na Katie Zaferes wa Amerika kwa zaidi ya dakika moja.

Hadi kufikia Julai 27, 2021, Bermuda ilikuwa ikishikilia rekodi ya kuwa taifa lenye idadi ndogo zaidi ya watu kuwahi kushinda medali ya Olimpiki baada ya bondia Clarence Hill kujizolea nishani ya shaba mnamo 1976.

Taifa hilo kwa sasa lina medali ya kwanza ya dhahabu.

Duffy aliyekataa fursa ya kuwakilisha Uingereza katika mashindano mbalimbali akiwa tineja, aliweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwahi kushindia Bermuda medali ya riadha alipotawala mashindano ya Jumuiya ya Madola mnamo 2018.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Wito wagonjwa wa kawaida wazuru hospitali nyinginezo idadi...

Helena Alcinda Panguana ampangua Mkenya Elizabeth Akinyi...