• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 5:50 AM
Vipusa wa Amerika watinga robo-fainali za soka ya Olimpiki licha ya kukabwa koo na Australia

Vipusa wa Amerika watinga robo-fainali za soka ya Olimpiki licha ya kukabwa koo na Australia

Na MASHIRIKA

MABINGWA wa dunia Amerika walifuzu kwa robo-fainali za Olimpiki licha ya kulazimishiwa sare tasa na Australia kwenye mchuano wa mwisho wa Kundi G mnamo Julai 27, 2021.

Vipusa wa Amerika walikamilisha kampeni za kundi lao katika nafasi ya pili baada ya Uswidi kuwapokeza New Zealand kichapo cha 2-0 na kumaliza kileleni kutokana na ushindi katika mechi zote tatu.

Huku Amerika na Uswidi wakifuzu kwa robo-fainali, Australia watalazimika sasa kusubiri kuona iwapo watabahatika kuwa miongoni mwa timu mbili zitakazosajili matokeo ya kuridhisha ila zikaambulia nafasi za tatu makundini.

Timu mbili za kwanza kutoka makundi matatu (E,F,G) zitafuzu kwa hatua ya nane-bora moja kwa moja.

Amerika walianza kampeni za Olimpiki wakijivunia rekodi ya kutoshindwa katika jumla ya mechi 44. Walijibwaga ugani kumenyana na Australia wakipania kuendeleza ubabe uliowavunia ushindi wa 6-1 dhidi ya New Zealand mnamo Julai 24 baada ya kulazwa 3-0 na Uswidi kwenye mchuano wa ufunguzi.

Australia walianza kwa kunyuka New Zealand 2-1 kabla ya kupigwa 4-2 na Uswidi.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Tufundishwe jinsi ya kuvua samaki na si kuletewa samaki,...

Red Carpet na South C United zakabana koo, Young City...