• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 10:08 PM
Red Carpet na South C United zakabana koo, Young City ikitoshana nguvu na Kipande FC

Red Carpet na South C United zakabana koo, Young City ikitoshana nguvu na Kipande FC

Na PATRICK KILAVUKA

KOCHA wa Red Carpet Meshack Onchonga Osore amesema timu ya South C United ilikuwa mwiba kwa timu yake lakini badiliko alilofanya kumuiNgiza mshambuliaji Antony Ochieng lilitengeneza mambo.

Timu hizi ziliambulia sare ya 3-3 baada ya timu yake kutoka nyuma 3-1 katika mechi ya Ligi ya Kanda ya FKF, Nairobi West uwanjani Kihumbuini (Jumapili). Magoli ya Carpet yalifungwa na Geofrey Alma (mawili) dakika ya 16 na 80 na mfumaji Antony Ochieng dakika ya 78 ilhali United walipachika kupitia Marach Kenyang dakika 14, Mark Mwangi dakika ya 43 na Patrick Keya dakika ya 75.

Naye kocha wa South C United Evans Ayeko alikiri kwamba, wapinzani walitumia dakika za mwisho za kipindi cha pili kudhoofisha safu ya ulinzi kwa kufanya mashambulizi na uvamizi uliowatatiza wanangome na kuachilia magoli mawili chini ya dakika mbili.

Benchi ya South C United ikiongozwa kocha Evans Ayeko wa kwanza kulia. Picha/ Patrick Kilavuka

Timu meneja wa South C United Steve Githinji aliongezea kwamba, mchezo ulikuwa mzuri japo wapinzani walimakinika na kuwa wabunifu kipindi cha pili na penaliti ambayo timu yao ilipoteza, iliwashusha moyo wachezaji wao.

Young City na Kipande FC zilicheza soka tamanifu na mechi ikatamatika kwa sare ya 2-2. Hii ilikuwa mechi ya Ligi ya Kaunti ya Shirikisho la Soka Kenya (FKF), Nairobi East uwanjani Kihumbuini. City ndiyo ilikuwa ya kwanza kutia kimiani dakika ya nne kupitia Priston Adeya kabla kufutwa dakika ya saba na mchezaji wa Kipande Kevin Manyengo na kufanya mambo kuwa 1-1 kipindi hicho.

Katika kipindi cha pili, Kipande FC ilijituma zaidi na kunako dakika ya 54 Brian Nyandieka alikuwa amecheka na wavu. Hata hivyo, City ilijizatiti kuwadhibiti wapinzani na dakika ya 77 ilikuwa imesawazisha kupitia Collins Nyambicha.

Katika mchuano wa kirafiki ambao uliandaliwa uga huo kabla mechi hiyo, timu ya Kangemi Veterans iliambilia sare ya 1-1 mbele ya Uthiru Veterans.

Kangemi ilifunga kupitia Cosmas Wanjiru na Uthiru ilifuta bao kupitia Eric Onchonga.

You can share this post!

Vipusa wa Amerika watinga robo-fainali za soka ya Olimpiki...

Wanasoka 10 wa Pwani kupigania nafasi Starlets U-20