• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 9:40 PM
Mzozo wa nyadhifa ODM watishia kuangusha chama

Mzozo wa nyadhifa ODM watishia kuangusha chama

Na SHABAN MAKOKHA

CHAMA cha ODM kipo katika hatari ya kupoteza umaarufu wake katika Kaunti ya Kakamega kutokana na mzozo kuhusu kugawanywa kwa nyadhifa mbalimbali kwenye matawi ya chama hicho.

Kutokana na tofauti hizo wanasiasa hao wametoa wito kwa Gavana Wycliffe Oparanya na Naibu wake Philip Kutima ambaye ni mwenyekiti wa chama katika kaunti hiyo waingilie kati ili kuhakikisha nyadhifa hizo zinagawanywa kwa usawa.

Kaunti ya Kakamega ina wabunge wawili pekee wa ODM ambao ni Justus Kizito wa Shinyalu na Johnstone Naicca wa Mumias Magharibi.

“Hatujafurahishwa na jinsi ambavyo kiongozi wa vijana wa ODM hapa Kakamega Moffat Mandela na Katibu Nabii Nabwera wanavyoendesha masuala ya chama. Mtindo wao wa uongozi unaua umaarufu wa chama,” akasema aliyekuwa mwenyekiti wa tawi ndogo la Mumias Magharibi Suleiman Odanga.

Mwanasiasa huyo pamoja na mwenzake Raziah Makokha wanadai kuwa matawi madogo ya Matungu na Mumias Magharibi yalionewa kwa kupokonywa nyadhifa muhimu ilhali ndizo ngome za ODM Kakamega.

“Mumias Magharibi imekuwa na mbunge wa ODM tangu chama hicho kianzishwe. Kwa hivyo tunafaa tupokezwe wadhifa wa mwenyekiti au katibu mkuu katika kaunti badala tu ya kutoa wajumbe,” akasema Bw Odanga.

Viongozi wapya wa ODM ni Bw Kizito aliyepokezwa mwenyekiti huku Lucas Radoli kutoka Mumias Mashariki akiwa Naibu Mwenyekiti.

Katibu Mkuu ni Nabii Nabwera (Lugari), Mwekahazina, Geoffrey Ommatera (Kwisero), Katibu Mkuu Mtendaji Naomi Shiyonga (Malava) naye Bw Mandela kutoka Mumias Mashariki akasalia kiongozi wa vijana.

Bw Makokha alisema kuwa inasikitisha kuwa nyadhifa za kiongozi wa vijana na naibnu mwenyekiti ziliendea Mumias Mashariki ambayo haijawahi kutoa mbunge wa ODM tangu Bw Washiali ahamie ANC na Jubilee mnamo 2013 na 2017 mtawalia.

You can share this post!

Wakulima wa viazi vitamu walalamikia bei duni

Sababu zilizofanya chama cha Jubilee kusambaratika