• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 6:55 AM
Waiguru awataka wakazi wa Kirinyaga wachukue tahadhari maambukizi ya Covid-19 yakipanda

Waiguru awataka wakazi wa Kirinyaga wachukue tahadhari maambukizi ya Covid-19 yakipanda

Na SAMMY WAWERU

GAVANA wa Kirinyaga Anne Waiguru ametahadharisha wakazi kuhusu ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona katika kaunti hiyo.

Bi Waiguru amewataka wenyeji kutilia maanani kanuni na sheria zilizopendekezwa na Wizara ya Afya kudhibiti msambao.

Alisema idadi ya vitanda vya kulaza wagonjwa vimepungua, kufuatia ongezeko la wagonjwa wa Covid-19.

“Kasi ambayo virusi vya corona Kirinyaga vinaenea inaogofya, baadhi ya vituo vya afya na hospitali vitanda vya kulaza wagonjwa vimejaa,” Bi Waiguru akasema.

“Tunazuru vituo mbalimbali vya afya, vilivyojaa wagonjwa tunaelekeza wengine katika hospitali ambazo zina nafasi,” gavana akaelezea, akihimiza wakazi kuchukua tahadhari na kujikinga kuambukizwa corona.

Kauli ya Waiguru imejiri wakati ambapo Wizara ya Afya inaendelea kuonya kuhusu maambukizi ya virusi hatari kutoka India, Delta Variant.

Kenya imeingia katika mkumbo wa nne wa maambukizi.

Mapema wiki hii, serikali ililegeza kamba masharti yaliyowekewa sekta ya huduma za matatu, ambapo wameruhusiwa kubeba asilimia 100 ya abiria.

Hatua hiyo inazua hofu, wataalamu wa masuala ya afya wakionya huenda ikachingia ongezeko la maambukizi ya corona na kusambaa kwa kasi.

You can share this post!

Duale ajitetea kwa madai alirejelea Kanisa Katoliki kama...

Kongamano la ugatuzi kuhudhuriwa na wachache kutokana na...