• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 3:34 PM
KINYUA BIN KING’ORI: Uchaguzi wa Zambia uwe kielelezo kwa mataifa ya Afrika

KINYUA BIN KING’ORI: Uchaguzi wa Zambia uwe kielelezo kwa mataifa ya Afrika

Na KINYUA BIN KING’ORI

Historia mpya imeandikishwa katika buku la demokrasia nchini Zambia na barani Afrika kwa jumla Kufuatia ushindi wa kiongozi wa upinzani Hakainde Hichilema katika uchaguzi mkuu uliofanyika majuzi.

Wengi walitarajia Rais wa taifa hilo, Edgar Lungu angalishinda uchaguzi huo kwa asilimia kubwa, kushindwa kwa rais aliye mamlakani ni tukio la kihistoria na miujza katika Bara la Afrika ambalo kwa muda mrefu wagombeaji wa upinzani wameishi kupoteza chaguzi katika njia inayoashiria kura zao ziliibwa au matokeo ya urais kuvurugwa na serikali inayotumia vibaya mamlaka kukandamiza wapinzani.

Baada ya tume ya uchaguzi nchini humo kutangaza Hakainde kuwa rais mteule kwa kuibuka mshindi kwa kuzoa kura nyingi, Rais Edgar Lungu ambaye kwa sasa ni rais anayeondoka alitangaza kukubali kushindwa na kumtakia salamu za pongezi hasimu wake kisiasa kwa ushindi wake huku akimtakia heri na ufanisi katika majukumu yake mpya.

Hakika, Rais huyo aliyeanguka nwanguko wa mende alionyesha heshima kwa kuheshiimu matokeo hayo na uamuzi wa wapiga kura wa na anafaa kupewa heko.

Maelfu kwa malaki ya Wazambia walijitokeza vijijini na mijini kushangilia ushindi huo. Tume ya uchaguzi nchini Zambia inastahili kupewa hongera kwa kuandaa mazingira bora yenye haki na uwazi wakati wa upigaji kura licha ya kukumbwa na changamoto nyingi pamoja na shinikizo kutoka kwa serikali.

Tume za uchaguzi katika mataifa mengine Afrika hasa Kenya ambapo tumesaza miezi 11 kufikai uchaguzi mkuu ujao, Tume ya Uchaguzi (IEBC) ikiongozwa na mwenyekiti Wafula Chebukati inafaa iwe tayari imeonyesha wazi mikakati wanayofanya kufaulisha maandalizi ya uchaguzi ujao 2022.

Tume hiyo inafaa kuiga tume ya uchaguzi ya Zambia kwa kujiandaa kuendesha na kusimamia uchaguzi wa 2022 kwa njia huru, haki na yenye uwazi na kuaminika ambayo wagombeaji wote wanaweza kukubali ushindi au ushinde bila usumbufu kwa kuridhishwa na jinsi uchaguzi wa Agosti 9, 2022 utakavyoendeshwa kwa uwazi.

Kushindwa kwa Rais Edgar licha ya serikali kutumia nguvu na rasilimali nyingi kumpigia kampeni huku wagombeaji wa upinzani akina Hichilema aliyeshinda wakihangaishwa kisiasa na kunyimwa mazingira bora na salama kuendesha kampeni zao kutwa kucha.

Lakini wananchi wengi wa Zambia walikuwa wamekataa kauli liwe liwalo watapigia kura kiongozi huyo wa upinzani, licha ya kutishwa na kutiwa hofu walifaulu kufanya maamuzi yao na kuleta mabadiliko yanayogusa mioyo ya wapenda demokrasia ulimwenguni.

Ushindi huo huenda usiwape tabasamu viongozi wa upinzani kama vile Bw Raila Odinga, ambaye tangu waingie handshake na Rais Uhuru Kenyatta amewatia imani wafuasi wake atakuwa mgombezi wa urais 2022 na kuna dalili huenda Rais Kenyatta akamuunga mkono kuwa mrithi wake.

Si kosa Raila au Naibu Rais Dkt William Ruto kujivunia kupendelewa na kiongozi wa taifa, ila itakuwa sawa na kushangilia kuanguka ikiwa atapofushwa kisiasa na kuhadaika na Rais Uhuru na nguvu za serikali zitamfaa pakubwa uchaguzi ujao 2022.

Kuna dhana mtu anayeonekana kupendelewa na serikali iliyo mamlakani huishia kushindwa vibaya. Licha ya serikali kutumia nguvu nyingi tumeona ikishindwa hata katika chaguzi ndogo zinazofanyika nchini.

Kwa vile Rais uhuru Kenyatta ameonyesha wazi kumuidhinisha kiongozi huyo wa upinzani kuwania urais mwaka ujao, huenda hatua hiyo ikamnyima Raila kura nyingi ikiwa atakaa kitako na kutarajia kura nyingi kutokana na ungwaji mkono wa Rais na serikali.

Funzo kuu Raila au mgombezi yoyote anayofaa kujifunza kutokana na uchaguzi wa Zambia ni kwamba, Licha ya Hakainde kushindwa kwa kura chache na Rais Lungu katika uchaguzi wa 2016 aliendelea kutekeleza majukumu yake kama kiongozi wa upinzani wala hakuona pupa ya kujiunga na serikali kupitia handshake au mapatano. Aliamini katika demokrasia, haki na usawa katika Jamii.

Aliishi kutetea akiwa wananchi wa Zambia akiwa upinzani bila kujali usumbufu, mahangaiko wala vitisho,ni ujasiri uso mfano kusimama kidete kama Hakainde katika nchi yenye utawala unaotishia uhai wa mfumo wa kidemkrasia kama Zambia, haikuwa rahisi na hatimaye amefanikisha juhudi zake kupitia kura za wananchi wengi waliomchagua.

Ni wazi mwanasiasa yoyote angalipenda kuimarisha umaarufu wake kisiasa ili kufaulisha ndoto zake lakini naomba Raila odinga achanuke mapema akome kutarajia miujza 2022, hii ni Kenya twaishi katika siasa za usaliti huenda 2022 usipate kura nyingi ikiwa utapumbazwa utapewa kura Kwa kuegemea nguvu za serikali tu kama ‘deep state’.

Uchaguzi ujao ukizidi kuwadia, Raila azinduke ajue kushinda au kushindwa uchaguzi wa 2022 itategemea mikakati yake mwenyewe kuwafikia wananchi akiwaomba kura Wala siyo ungwaji mkono wa Rais au serikali.

Wananchi ndio wenye kura kuchagua wamtakaye Katika nyadhifa zote kuanzia udiwani hadi urais bora tu tume ya IEBC itekekeze wajibu wake Kwa ustadi, huru na haki na kwa mujibu wa Sheria za ucha

You can share this post!

WANDERI KAMAU: Tukomeshe unyama huu kwa vijana wa Kenya

Wanaomezea mate ugavana waongezeka